September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amteua bosi wa zamani SADC kuwa mbunge

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Stergomena Tax, kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya Jaffari Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu aliyoitoa leo Ijumaa, tarehe 10 Septemba 2021, imesema Dk. Tax ataapishwa kwa mujibu wa sharia na taratibu za Bunge.

Rais Samia amemteua, Dk. Tax takribani wiki mbili zimepita tangu alipomaliza muda wake wa miaka nane ya kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Uteuzi huo kwa Dk. Tax ni wa pili kufanywa kwake na Rais Samia kwani tarehe 13 Mei 2021, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi.

Dk. Tax ambaye ni raia wa Tanzania, alianza kutumikia jumuiya hiyo mwaka Septemba 2013, baada ya kuteuliwa katika mkutano wa 33 wa SADC uliofanyika, Lilongwe nchini Malawi.

Dk. Tax, amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki ya Tanzania kati ya Novemba 2008 hadi August 2013, ikiwa ni katika utawala wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

error: Content is protected !!