Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Gwajima ahojiwa, kurudi tena kikaangoni Jumatano
Habari za SiasaTangulizi

Askofu Gwajima ahojiwa, kurudi tena kikaangoni Jumatano

Askofu Josephat Gwajima akiwasili viwanja vya Bunge tayari kuhojiwa na Kamati ya Bunge
Spread the love

 

MBUNGE wa Kawe, mkoani Dar es Salaam (CCM), Askofu Josephat Gwajima, ameanza kuhojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, dhidi ya tuhuma zinazomkabili za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya mhimili huo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbunge huyo wa Kawe, ameanza kuhojiwa leo Jumatatu, tarehe 23 Agosti 2021 na kamati hiyo katika ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya mahojiano hayo kuahirishwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka, amesema shauri hilo limeahirishwa hadi Jumatano hii, ambapo shahidi huyo ataendelea kutoa utetezi wake.

“Tumemsikiliza, tumemruhusu ameenda lakini shauri lake bado linaendelea. Tutakutana naye Jumatano mchana tarehe 25 Agosti 2021,” amesema Mwakasaka.

Alipoulizwa kwa nini shauri hilo litasikilizwa zaidi ya siku moja, Mwakasaka amesema hatua hiyo inatokana na mijadala iliyoibuliwa katika mahojiano hayo.

“Kwanza kama mnavyofahamu tumekutana naye mchana, hili suala halina sababu tofauti sana kwamba kwa nini iwe siku mbili, inawezekana ikawa siku mbili, tatu au nne inategemea mjadala unavyokwenda na shahidi mwenyewe jinsi yeye anavyojieleza,” amesema Mwakasaka.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Maadili ya Bunge ameongeza: “tunampa uhuru wa kutosha kuzungumza, unapompa shahidi uhuru kuzunguma unaweza usimamlize kumhoji. Ndiyo maana tunaenda siku ya pili, ni taratibu za kawaida.”

Baada ya kuulizwa hatua gani zitakazochukuliwa na Bunge dhidi ya Askofu Gwajima, baada ya mahojiano hayo, Mwakasaka amesema suala hilo hawezi kulizungumzia.

“Katika hatua hii siwezi kuongelea adhabu, sababu bado kamati hii hatujafikia hatua hiyo kwamba kwa sasa kuna adhabu ya aina fulani na hata kama ingekuwepo bado mimi mwenyekiti si msemaji kwa niaba ya Bunge bali spika ndio mleta shauri kwa mujibu wa kanuni,” amesema Mwakasaka.

Hata hivyo, Mwakasaka amesema ziko adhabu za aina nyingi anazochukuliwa mbunge baada ya kubainika na hatia.

“Tunaendelea naye, huwezi kusema katika hatua hizi kwamba unaweza kumchukulia hatua gani. Sababu sis adhabu ya aina moja inayotolewa, zipo adhabu za aina mbalimbali na hata mtu huwa anasamehewa pia,” amesema Mwakasaka.

Mwakasaka amesema, baada ya kamati hiyo kumaliza kazi yake, watapeleka taarifa ya mahojiano hayo na mapendekezo yake kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa ajili ya hatua nyingine.

“Na tukimaliza tunampelekea yeye, sisi tumepata nini na nini mapendekezo yetu tunayapeleka kwake na yeye ndio mwenye shauri,” amesema Mwakasaka

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!