Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Gwajima, Jerry Silaa waondolewa kwenye kamati
Habari za SiasaTangulizi

Askofu Gwajima, Jerry Silaa waondolewa kwenye kamati

Spread the love

 

ASKOFU Josephat Gwajima ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kawe na Jerry Silaa wa Jimbo la Ukonga mkoani Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wameondolewa kwenye kamati hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa leo Agosti 24, 2021 hadi itakapoamuliwa vinginevyo Bungeni jijini Dodoma.

Askofu Josephat Gwajima na Jerry Silaa wameitwa mbele ya kamati hiyo wakituhumiwa kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Kamati hiyo ina jumla ya wajumbe 24 wakiwamo Gwajima na Silaa na sasa imebaki na wajumbe 22 baada ya hatua hiyo.

Askofu Gwajima alianza kuhojiwa jana tarehe 23 Agosti, 2021 na kamati hiyo kwa zaidi ya saa mbili na tarehe 25 Agosti, 2021 ataendelea kuhojiwa wakati Silaa anahojiwa leo mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Emmanuel Mwakasaka.

Mwakasaka amesema unapotuhumiwa mara nyingi, wewe ndio mshtakiwa.

“Hivyo zipo taratibu zinafuata. Kama wewe ni mtuhumiwa huwezi kuwa hakimu kwenye kesi yako mwenyewe,”amesema Mwakasaka huku akiongeza kuwa, tayari wajumbe hao wameondolewa katika kamati.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

error: Content is protected !!