June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia, Kikwete kumshuhudia Rais mteule Zambia akiapishwa

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuondoka nchini kesho tarehe 24 Agosti, 2021 kuelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Zambia, Hakainde Hichilema. Anaripoti Mwandishin Wetu … (endelea).

Sherehe za uapisho wa Rais huyo mteule wa saba wa Zambia zitafanyika katika Uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium), Jijini Lusaka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo tarehe 23 Agosti, 2021, katika msafara wake Rais Samia ataongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka.

Hakainde Hichilema

Wengine ni Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa CCM Ndugu Maudline Cyrus Castico, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM -Mizengo Peter Pinda, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mzee Kombo Hassan Juma, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mzee Henry Daffa Shekifu, na Mbunge wa Jimbo la Mtera na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe. Livingstone Joseph Lusinde.

Aidha, Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete atashiriki katika sherehe hizo akiwa kiongozi wa timu ya waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Madola.

error: Content is protected !!