Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yajitosa tozo za miamala ya simu, yampongeza Rais Samia
Habari za Siasa

CCM yajitosa tozo za miamala ya simu, yampongeza Rais Samia

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejitokeza kumpongeza Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan, kwa kusikia malalamiko ya wananchi juu ya tozo za miamala ya simu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ni baada ya tozo hizo kuanza kukatwa tarehe 15 Julai 2021, ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Fedha iliyopitishwa na Bunge la Bajeti kisha kusainiwa na Rais Samia, ili kuanza kutumika.

Jana Jumatatu, tarehe 19 Julai 2021, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba alisema, Rais Samia ameagiza kufanyiwa kazi kwa malalamiko hayo.

           Soma zaidi:-

Leo Jumanne, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakutana katika kikao cha wizara husika kushughulikia malalamiko hayo.

Mara baada ya Waziri Mwigulu kutoa taarifa hiyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilijitokeza mbele ya waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, kuzungumzia maagizo hayo ya Rais Samia.

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alimpongeza Rais Samia ambaye ni Menyekiti wa CCM, kwa usikivu wake kwa wananchi anaowaongoza na kuamua suala la tozo kutizamwa upya.

Alisema kwa hatua hiyo Rais Samia, ameendelea kuwathibitishia Watanzania na dunia kwa ujumla kuwa ni kiongozi imara, mzalendo, shupavu na mwenye dhamira ya kweli kwa watu wake anaowagonza ili kuwatoa na kujikwamua na umasikini.

“Chama kinatoa maelekezo kwa Serikali pamoja na kupitia upya tozo hii ya miamala ya simu, lakini pia iandae utaratibu wa kupitia upya sera na sheria ya kodi na kuratibu ubunifu utakaoibua vyanzo vipya vya kodi ili kupunguza mzigo mzito kwa wananchi,” alisema Shaka

Shaka alisema “chama kinawasisitiza wananchi kuendelea kuiamini na kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia na kuendelea kuona fahari ya kulipa kodi kwa hiyari na uaminifu kwa maendeleo endelevu ya taifa letu.”

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinachoongoza Serikali ya Tanzania, kina zaidi ya wabunge asilimia 90 ambao ndiyo walijadili na kupitisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/22 pamoja na Sheria ya Fedha yam waka 2021.

1 Comment

  • Acheni unafiki. Je wakati sheria ya kodi inapitishwa nyinyi wa CCM na wabunge wenu mbona mlishagilia? Leo eti mnapongeza kufikiria upya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!