MUHAMMAD Bin Salman, Mwanamfalme wa Saudia, ameidhinisha kutolewa fedha milioni 3.74 za riyali, sawa na dola milioni 1 za kimarekani, ili zigawiwe kwa vijana 200 kama ruzuku ya kuoa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Mtandao huo, umeripoti kwamba, Gazeti la Serikali la Saudi Arabia, limesema fedha hizo zitagawanywa kwa vijana wa kiume na wa kike kote nchini humo.
Limesema agizo la Mwanamfalme huyo ni katika juhudi za kuwasaidia yatima wenye ulemavu na watu wenye ulemavu ambao wamekuwa na shida ya kuoa.
Katika awamu ya kwanza ya mpango huo, riyali milioni 250 za msaada zilisambazwa, kwa watu zaidi ya 26,000 kutoka maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Licha ya kupewa fedha, vijana watafundishwa jinsi ya kutumia fedha.
Mpango wa Mwanamfalme Muhammed Bin Salman ulianzishwa kwa lengo la kuimarisha uchumi na jamii ya watu wa nchi hiyo kuboresha maisha ya watu.
Leave a comment