Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko “Mkapa alidhibiti Ukimwi, aligusa maisha ya Watanzania Mil. 20”
Habari MchanganyikoTangulizi

“Mkapa alidhibiti Ukimwi, aligusa maisha ya Watanzania Mil. 20”

Hayati Benjamin Mkapa
Spread the love

ALIYEKUWA Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa, ametajwa kuwa na mchango mkubwa katika kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatano, tarehe 14 Julai 2021 na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro, katika kongamano la kumbukizi ya Mkapa, lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.

Mkapa aliyeiongoza Tanzania kwa miaka 10 mfululizo, kuanzia 1995 hadi 2005, alifariki dunia tarehe 24 Julai 2020, mwili wake ulizikwa nyumbani kwao Lupaso mkoani Mtwara, tarehe 29 Julai mwaka jana.

Dk. Senkoro amesema kuwa, Mkapa alipokuwa madarakani, aliiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuanzisha kliniki za waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi, pamoja na kutoa dawa za ARV zinazofubaza Virusi vya Ukimwi (VVU).

Amesema, Mkapa aliweka mikakati mbalimbali ya kupambana na Ukimwi, iliyowezesha kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo, kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, hasa wakati wa kujifungua.

“Mkapa alikuwa bingwa katika mapambano ya Ukimwi, hasa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kutokana na hilo,  alitambulika bingwa ulimwenguni kwa kuanzisha kliniki za wagonjwa wa Ukiwmi na kutoa dawa,” amesema Dk. Senkoro.

Dk. senkoro ameongeza “ Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kuanzisha utoaji dawa kwa waathirika wa Ukimwi hasa wajawazito. Hayo ni mafanikio yaliyoacha alama ya uongozi wake.”

Kwa mara ya kwanza, Ukimwi uligundulika mkoani Kagera, mwanzoni mwa miaka ya 1980.

2003 alipokuwa madarakani, Mkapa alianzisha Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi wa miaka mitano (2003-2007), mkakati huo uliandaliwa na Tume yta Taifa ya Kudhibiti Ukiwmi (TACAIDS).

Mbali na kutoa mchango mkubwa katika kudhibiti maambukizi na vifo vitokanavyo na Ukimwi, Dk. Senkoro amesema, kupitia Taaasisi yake, Mkapa alifanikiwa kugusa maisha ya Watanzania milioni 20 , kupitia miradi ya sekta ya afya, iliyotekelezwa kwa muda wa miaka 15, tangu ianzishwe.

“Watu takribani milioni 20 waliguswa moja kwa moja na kwa njia nyingine, kupitia miradi ya afya tuliyofanya ndani ya miaka 15 tangu taasisi ilipoanzishwa,” amesema Dk. Senkoro.

Amesema, taasisi hiyo ilifadhili wanafunzi 736 waliosomea kada za afya, ambao baadhi yao imewaajiri huku wengine wakiajiriwa serikalini.

Pia, taasisi hiyo ilitoa vifaa vya maabara na vyumba vya upasuaji zaidi ya 500, Tanzania Bara na Zanzibar. Amesema hadi Mkapa anafariki dunia, taasisi hiyo imejenga  vituo vya afya zaidi ya  5,000 nchi nzima.

Taasisi iliyoanzishwa tarehe 13 Aprili 2006, imeajiri watumishi wa afya zaidi ya 900 nchi nzima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!