Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yaanzisha utaratibu kuweka akiba
Habari Mchanganyiko

NMB yaanzisha utaratibu kuweka akiba

Spread the love

 

BENKI ya NMB imeanzisha huduma maalum kwa wateja wao kujiwekea akiba kila wanapofanya mialama. Anaipoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Huduma hiyo ya kwanza nchini, inajulikana “Spend to save”- miamala yako ni akiba yako, imezinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na maofisa waandamizi wa benki hiyo.

Aidha, huduma hiyo yenye lengo la kuwahamasisha wanancji kujiwekea akiba, ni kwa ajili ya akaunti binafsi, akaunti za chap chap na akaunti za mwanachuo.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi, alisema “Spend to Save” inadhihirisha ubunifu wa hali ya juu wa benki hiyo na uongozi wake wa kuanzisha suluhisho wezeshi za kibenki.

Alisema, huduma ya “Spend and Save” inapatikana kwa mteja kujisajili kupitia zaidi ya ATM 8,000 za benki hiyo zilizosambaa nchi nzima na kuweka malengo kwa asilimia ya kila muamala anaoufanya.

Mponzi alisema, kiasi kitakachokatwa kwa ajili ya akiba ni kati ya asilimia mbili hadi kumi ya kila muamala utakaofanyika na miamala itakayohusika ni ile inayofanywa kupitia ATM, POS, NMB Direct au NMB Mkononi.

“Hili ni jambo kubwa kipindi hiki tunapowakumbusha Watanzania na wateja wa NMB kujitunzia akiba kwa maisha ya baadae,” alisema Mponzi.

“Huduma hii ni ya kwanza na ya aina yake kuwahi kutokea nchini Tanzania ambapo mteja anajitunzia fedha zake kupitia miamala yake anayoifanya iwe kununua kitu, kutoa fedha kutoka kwenye akaunti yake au hata kutuma fedha,” alisema.

Mponzi alisema, benki hiyo imeanzisha utaratibu huo baada ya kugundua wateja wake wengi hawana tabia ya kuweka akiba na hivyo kuona umuhimu wa kuwaletea huduma ambayo itawasaidia kuweka akiba mara kwa mara na kwa malengo.

Aidha, uzuri wa huduma hiyo ni mteja kuweza kutoa fedha zake kutoka kwenye waleti na kuzirudisha kwenye akaunti muda wowote na atakapofanya hivyo ataruhusiwa kutoa mpaka asilimia 50 ya fedha iliyohifadhiwa.

Pia, mteja anaweza kujitoa kwenye wallet na fedha zilizohifadhiwa zitarudishwa kwenye akaunti mama.

“Huu ni muendelezo wa huduma ambazo NMB tumekuwa tukianzisha ili kusaidia wateja wetu kwa kutoa suluhisho za huduma za kibenki zenye tija hapa nchini na kutufanya kinara wa kufanya hivyo,” alisema Mponzi

Naye Mkuu wa Idara ya Bidhaa, Aloyse Maro, alisema huduma hiyo mpya pia inaongeza namna bora ya kuwahudumia wateja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!