May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mjane wa Rais Haiti ashtumu mauaji ya mmewe

Martine Moise, mke wa aliyekuwa Rais wa Haiti, Jovenel Moise

Spread the love

 

MARTINE, mjane wa Rais aliyeuawa wa Haiti, Jovenel Moise ameshutumu mauaji ya mumewe kwa kusema maadui walilenga kusitisha mabadiliko ya demokrasia. Inaripoti Mitandao ya kijamii…(endelea).

Akizungumza katika video iliyochapishwa katika mtandao wa Twitter, Martine Moise amesema, mumewe alilengwa kwa ajili ya siasa.

Hayati Moise, wakati wa utawala wake, aliwakasirisha wanasiasa wa upinzani kwa kujaribu kuleta mabadiliko katika mikataba ya serikali na siasa na alipanga kufanyika kura ya maoni ya kubadilisha katiba ya Haiti, iliyolenga kumpa rais madaraka makubwa.

Rais Moïse aliuawa tareje 7 Julai 2021, ikidaiwa kuwa mauwaji hayo yaliendeshwa na mamluki 28 kutoka mataifa ya kigeni.

Mjane huyo ambaye pia alijeruhiwa katika shambulio hilo lililotokea nyumbani kwao, na kusafirishwa hadi Miami, nchini Marekani kwa ajili ya matibabu.

“Ghafla, mamluki waliingia nyumbani kwangu na kumuua mume wangu kwa risasi,” anasema katika video hiyo, akielezea wakati ambapo washambuliaji walimuua mumewe.

Alisema “kitendo hiki hakina jina kwa sababu lazima uwe mhalifu sugu kumuua rais kama Jovenel Moïse, bila hata kumpa nafasi ya kusema neno moja.”

Alidai kama mumewe alikuwa akilengwa kwa sababu za kisiasa – haswa, akitaja kura ya maoni juu ya mabadiliko ya katiba ambayo ingeweza kumpa rais nguvu zaidi.

Watu hao ambao hawajulikani alisema, “wanataka kuua ndoto ya rais.”

“Ninalia, ni kweli, lakini hatuwezi kuiacha nchi ipotee,” alisema “Hatuwezi kuruhusu damu ya Rais Jovenel Moïse, mume wangu, rais wetu ambaye tunampenda sana na ambaye alitupenda sisi, kupita bure.”

Moïse, mwenye umri wa miaka 53, alikuwa rais wa Haiti, taifa maskini zaidi katika Amerika, tangu 2017.

Wakati wake katika ofisi ulikuwa mgumu kwani alikabiliwa na tuhuma za ufisadi na kulikuwa na maandamano mengi katika mji mkuu na miji mingine mapema mwaka huu.

Uchaguzi wa bunge ulipaswa kufanywa Oktoba 2019 lakini mizozo imechelewesha, ikimaanisha Moïse alikuwa akitawala kwa amri. Alikuwa amepanga kufanya kura ya maoni juu ya mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa mnamo Septemba 2021.

error: Content is protected !!