Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Gwajima aibana Serikali bungeni kisa wavuvi
Habari za Siasa

Askofu Gwajima aibana Serikali bungeni kisa wavuvi

Spread the love

 

MBUNGE wa Kawe mkoani Dar es Salaam, Askofu Josephat Gwajima, amehoji lini Serilkali itapeleka boti za doria jimboni humo, kwa ajili ya kuokoa maisha ya wavuvi wadogo pindi wanapopata ajali.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Askofu Gwajima amehoji hayo leo Jumatatu, tarehe 7 Juni 2021, katika kipindi cha maswali na majibu, bungeni jijini Dodoma.

“Kwa kuwa karibu wenyeji wote wa Kawe wanajishughulisha na uvuvi mdogo, hasa wa mitumbwi na mara nyingi hutokea ajali hasa wakati wa usiku na kuhatarisha maisha yao. Lini Serikali italeta boti ndogo kwa ajili ya kuokoa, inapotokea madhila ya namna hiyo?” Amesema Askofu Gwajima.

Pia, Mbunge huyo wa Kawe, amehoji lini Serikali itakuwa na mpango maalum wa kutoa mikopo kwa wavuvi wadogo jimboni humo, ili kuboresha uvuvi wao.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema Serikali iko kwenye mkakati wa kutoa vyombo vya doria baharini, ili kuwasaidia wavuvi wanaopata matatizo wakiwa kwenye shughuli zao.

“Kuhusu usalama wa wavuvi na uokozi pale wanapopata madhila mbalimbali baharini, Serikali kwa pamoja Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Police Marine (Polisi wa majini), zote zinafanya kazi kwa pamoja,” amesema Ulega.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega

Ulega ameongeza “na hivi sasa tuko katika mkakati kuhakikisha panapatikana vyombo vinavyofanya kazi hiyo ya doria, jambo hili linaratibiwa vyema na Ofisi ya Waziri Mkuu.”

Kuhusu mikopo kwa wavuvi, Ulega amesema katika mwaka wa fedha wa 2021/22, Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi wadogo, ikiwemo kuwapatia mashine za boti.

“Kuhusu mikopo nataka nikuhakikishie tumejipanga vyema na katika bajeti yetu ya 2021/22, nikukaribishe kwa ajili ya vikundi wapate mashine za boti,”

“ Na kujiunga katika vikundi vitakavyowasaidia kutengeneza vichanja vya ukashauji samaki na hata kutengeneza mashine za kuzalisha barafu, wauziane wenyewe kwa ajili ya kuondosha tatizo la upotevu wa mazao,” amesema Ulega .

Aidha, Ulega amesema Serikali ina mpango wa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), kutoa leseni kwa meli kubwa za watu binafsi, pamoja na kujenga bandari ya uvuvi katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, ili kuimarisha uvuvi wa Bahari Kuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!