Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Sabaya noma, jumba la mateso…
Habari MchanganyikoTangulizi

Sabaya noma, jumba la mateso…

Lengai ole Sabaya
Spread the love

 

JUMBA la kutesea watu, maarufu kama Golgota, linalomilikiwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya, limegundulika rasmi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Jumba hilo la mateso, ambalo Sabaya alikuwa akilitumia kutesea watu mbalimbali aliokuwa ametofautina nao, lipo katika eneo la Sakina mjini Arusha.

Golgota ni kituo cha mwisho ambacho Yesu Kristo aliteswa na kusulubiwa.

Sabaya alilitumia eneo hilo ambalo ni nyumba (apartment), aliyopangishiwa rafiki yake wa kike (girlfriend), kwa gharama ya Sh. 200,000 kwa mwezi.

Mmiliki wa nyumba Anthony Kabantega, amethibitisha madai kuwa nyumba yake imekuwa ikitumiwa na Sabaya, kutesea watu mbalimbali.

“Nikweli kwamba nilipokea taarifa za watu mbalimbali kuteswa katika nyumba niliyompagisha rafiki wa kike wa Sabaya…”

Kupatikana kwa taarifa hizi, kumekuja siku tatu tangu Sabaya na wenzake watano, wafikishwe mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Arusha na kusomewa mashtaka matano, yakiwamo kumiliki magenge ya uhalifu, unyang’anyi wa kutumia silaha na utatishaji fedha.

Mashtaka karibu yote yanayomkabili, hayana dhamana kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Mahakama imepanga tarehe 18 Juni, kwa Sabaya kurejea tena mahakamani kusikiliza kesi zinazomkabili.

Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema la leo Jumatatu tarehe 7 Juni 2021, utaona jinsi mmiliki wa nyumba alivyosota kupata kodi yake, bosi wa Takukuru akizungumzia uchunguzi zaidi wa Sabaya na jinsi mamilioni yanayodaiwa kuwa ya Sabaya walivyokutwa benki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 120 za DMDP zaibadilisha Ilala, wananchi watoa ya moyoni

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 120.7 zimetumiwa na Halmshauri ya Jiji...

error: Content is protected !!