WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (Tehama), Dk. Faustine Ndugulile ameitaka, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuboresha mifumo mbalimbali ya usimamizi wa huduma za mawasiliano ili kuhakikisha usalama na ubora wa huduma nchini, unakuwepo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Dk. Ndugulile, alitoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki, mara baada ya kutembelea mifumo hiyo makao makuu ya TCRA mkoani Dar es Salaam na kupokewa na viongozi mbalimbali wa mamlaka hiyo akiwemo Mkurugenzi wake Mkuu, Dk. Jabiri Bakari.
Alisema wananchi wanatarajia kupata huduma bora zenye usalama.
“Upatikanaji wa huduma bora, za uhakika na salama ni jambo la msingi sana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa” alisema Dk. Ndugulile.
Waziri huyo, aliipongeza TCRA kwa ubunifu wa kujenga mifumo wezeshi kwa huduma mbalimbali za mawasiliano nchini, ambapo uboreshaji wake ni muhimu.
Baadhi ya mifumo aliyotembelea ni Mfumo wa Usimalizi na Udhibiti wa Masafa ya Redio na Televisheni na Kituo cha Kuratibu Majanga ya Kimtandao (TZ-CERT).
TZ-CERT pia itatoa ushuri wa kitaalam namna bora wa kudhibiti na kupambana ya majanga mbalimbali ya kimtandao kwa taasisi na makampuni mbalimbali nchini Tanzania.
Waziri pia alitembelea kituo cha huduma kwa wateja ambapo alihimiza TCRA kuendeza kushirikiana na taasisi zingine zikiwemo za kiudhibiti kama Banki Kuu ya Tanzania (BoT).
Leave a comment