Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia atoa maagizo korosho ipitie bandari Mtwara
Habari Mchanganyiko

Rais Samia atoa maagizo korosho ipitie bandari Mtwara

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, ameagiza korosho zote zinazozalishwa mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia badari ya Mtwara. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya serikali kufanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.

Majaliwa amesema hayo leo Jumapili, tarehe 6 Juni 2021, wakati wa kikao na wadau wa zao la korosho kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sea View, iliyopo mjini Lindi.

Amesema Rais Samia amewaagiza viongozi wa bandari wapitie tozo zote zinazowakwaza wasafirishaji ili kuwavutia kuitumia bandari hiyo “tunataka wasafirishaji watumie bandari hii kusafirisha korosho kuanzia na msimu huu.”

Aidha, Waziri Mkuu amesema, wakulima wakubali kupokea pembejeo kulingana na mahitaji yao na watalipia kulingana na idadi ya mifuko waliyochukua na sio Sh.110 kwa kila kilo kama inavyelezwa “kila kilo ni gharama mno, lengo letu ni kuendelea kumpungumzia mzigo mkulima, msiogope kuchukua pembejeo.”

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Majaliwa ametoa wito kwa wakulima wa zao la Korosho kuwa na utaratibu wa kubangua korosho ili kupata faida zaidi badala kuziuza bila kuzibangua “tungebangua wenyewe tungepata faida kubwa sana, wenye viwanda panueni viwanda vyenu na kukuza mitaji na wakulima wadogo endeleeni kubangua ili kuongeza thamani ya korosho zetu.”

Amesema, Serikali itaendelea kuwaunga mkono wadau wote wa korosho nchini katika kufanikisha mkakati huo ikiwemo kutengeneza mashine za ubanguaji kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) “ni vyema tujikite kwenye ubanguaji kuliko kuisafirisha nje ya nchi ikiwa ghafi, tumeandaa mfumo mzuri na Rais wetu ameendelea kusisitiza katika ujenzi wa viwanda.”

Akizungumzua tozo ya unyaufu, Majaliwa amesema, tozo hiyo haikubaliki kwa kuwa haina uhalisia kwani hata sheria na kanuni kwenye Wizara ya kilimo haitambui unyaufu. “tusisikie makato ya unyaufu kwasababu yanawafanya wanunuzi wahisikuwa wanaonewa, viongozi wa Serikali tusimamie hilo, hatutaki kusikia kuhusu tozo ya unyaufu”

Vilevile, Waziri Mkuu amesema Serikali inaweka mpango wa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Afisa Ugani mmoja atakayesaidia kutoa elimu kwa wakulima juu ya namna bora ya kusimamia mazao yao ili kuongeza tija.

“Wakulima wanakosa elimu ya namna ya kuliendesha zao hili, maafisa kilimo mlioko maofisini tokeni muende vijijini kuwaelimisha wakulima namna bora ya kulima mazao, wakati wote mnatakiwa kuwa shambani kuhakikisha wakulima wanalima kwa kuzingatia miongozo ya kilimo bora.”

Naye Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema, wizara hiyo itaendelea kubuni na kusimamia mikakati itakayoongeza tija katika zao la korosho kwa kutoa pembejeo sahihi na kwa wakati lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya masoko duniani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Taleck amesema, atashirikiana na viongozi wa mikoa ya Ruvuma na Mtwara kuhakikisha kwamba minada yote ya korosho inafanyika kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mbunge wa Jimbo la Tandahimba (CCM), Katani Ahmad Katani amesema, amefarijika na kauli ya Serikali kuhusu korosho zote kusafirishwa kupitia bandari ya Mtwara kwani itasaidia kuongeza fursa za maendeleo katika mikoa ya kusini.

Akichangia katika mjadala huo, Mkulima wa Korosho kutoka Tunduru, Shaibu Hassan amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuondoa tozo ya shilingi 110 kwa kila kilo moja ya korosho ghafi inayouzwa kwa ajili ya pembejeo.

“Kero yetu kubwa ilikuwa ni kilo moja ya pembejeo uchukue salfa au usichukue, huu ndio ujumbe mzito ambao Mama Samia ametupatia sisi wakulima wa korosho,” amesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!