Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali kuajiri walimu 6,949, wataalamu afya 2,726
Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali kuajiri walimu 6,949, wataalamu afya 2,726

Spread the love

SERIKALI imetangaza nafasi za ajira kwa walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Nafasi hizo zimetangazwa leo Jumapili tarehe 9 Mei 2021, na Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

Ummy amesema nafasi za ajira kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ni 6,949, huku za watumishi wa kada za sekta ya afya zikiwa ni 2,726.

“Serikali imetoa kibali cha nafasi za ajira ya walimu 6,949 wa shule za msingi na sekondari na watumishi 2,726 wa kada mbalimbali za sekta ya afya,” amesema Ummy.

Waziri huyo wa TAMISEMI amesema nafasi hizo zimetangazwa kwa ajili ya kujaza pengo lililoachwa na watumishi waliokoma utumishi,  kutokana na sababu mbalimbali.

“Nafasi hizo zimetangazwa ili kujaza nafasi wazi za watumishi waliokoma utumishi kutokana na sababu mbalimbali kama vifo, kuacha kazi, kufukuzwa kwenye utumishi na kustaafu,” amesema Ummy.

Ummy amesema mchakato wa kuomba ajira hizo umekamilika, na kwamba wahitaji wanaweza kuomba nafasi hizo kuanzia leo hadi tarehe 23 Mei 2021.

“Taratibu za kuanza mchakato wa kuomba ajira umekamilika, waombaji wenye nia wanaweza kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira TAMISEMI, kuanzia leo tarehe 9 hadi 23 Mei, 2021,” amesema Ummy.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

error: Content is protected !!