Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kuanza operesheni nchi nzima
Habari za Siasa

Chadema kuanza operesheni nchi nzima

Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kinakusudia kuanza operesheni nchi nzima. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na Watanzania kupitia mitandao ya kijamii leo tarehe 11 Aprili 2021, Mbowe amesema, chama hicho kitafanya operesheni ili wananchi wajue hatma ya nchi yao.

“Chama chetu kitaanza operesheni maalumu ili Watanzania wajue hatma ya nchi yao, kwasababu za kimkakati na kiuslama itoshe kuishia hapo.

“Wanachama wetu popote walipo wajiandae, tunataka kukipekea chama katika viwango viya vya kitaifa na kimataifa, sisi sio watu wa kukatishwa tamaa,” amesema Mbowe.

Akiongozwa na kauli ya kamwe, kamwe isijirudie (utawala wa Rais John Magufuli), Mbowe amesema mpango wa kuzunguka nchi nzima, uliwekwa na chama hicho tangu Januari mwaka huu, na kwamba wakati wanajiweka sawa ‘Magufuli (Rais Magufuli), akatangulia mbele ya haki.’

Amesema, kutokana na hilo (Rais Magufuli kufariki dunia), chama hicho kinajipanga tena na namna ya kuanza kuzunguka nchi nzima, awali operesheni hiyo amesema ilipaswa kuanza mwezi huu (Aprili).

Kiongozi huyo amesema, suala la kusimamia demokrasia ya nchi, sio la wanasiasa pekee, na kwamba ni ulegevu wa wananchi umelifikisha Taifa kufika hapa lilipo.

“Tumefika hapa kwa kuwa tumekuwa legelege, ni jukumu letu wote kusimamia demokrasia,” amesema Mbowe huku akisistiza uhitaji wa Katiba Mpya si suala la hiyari ya watawala.

“Uhitaji wa Katiba Mpya hauhitaji kuwa utashi wa rais na chama chake. Katiba ni msingi, ni roho ya Taifa. Uhitaji wa Katiba Mpya haupaswi kuwa kwa rais ama chama chake.

“Hatuhitaji mjadala wa kuwa na Katiba, mjadala umeishafungwa, na ndio maana tulianza mchakato wa Katiba,” amesema Mbowe.

2 Comments

  • Asante ndugu mbowe kwanza maliza mpasuko wa chadema alafu ndio ifanye mzungo usionama kwa watu wenye maana ukienda ulaiya unakuenda na familya yako kuzungu tanzania uzunguke na walala oi hakuna tena wakumdaganya endeleaza maishA yako kwa faida yako chadema isiwe ngao yako

  • Baada ya kukosa ubunge ndo unaona mpasuko! Chama hiki sio kile chama cha 2014 kushuka chini, sio kile chama kilichokua kinapinga ufisadi, sio chama tena bali ni kagenge ka kiuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!