May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wabisha hodi Ikulu

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema chama hicho kimemwandikia barua Rais Samia Suluhu Hassan, kuomba kukutana naye. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Amesema, dhamira ya barua hiyo ni kutaka kujadili mustakabali wa Taifa, kuhusu maendeleo ya kisiasa, uchumi na kijamii.

Taarifa hiyo ameitoa leo tarehe 11 Aprili 2021, wakati akilihutubia Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mbowe amesema, hayo wakati akizungumzia wito wa Rais Samia wa Taifa kuziweka tofauti zao pembeni na kuwa wamoja, alioutoa baada ya kuapsihwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021, akichukua mikoba ya Hayati Dk. John Magufuli, aliyefariki dunia akiwa madarakani tarehe 17 Machi 2021.

“Mama yetu Samia alizungumza maneno haya na Taifa lilimsikia,  kwa niaba ya Chadema nimeuandikia barua Mama Samia  pamoja na mambo mengine,  nimueleza maneno yake haya yamegusa maneno watu wengi yenye hofu ya Mungu ikiwemo sisi.

” Hata hivyo, sisi Chadema  bado mioyo yetu imebubujikwa na damu kwa tuliyopitia na tunayoendelea kupitia,” amesema Mbowe.

Pia amesema, kama maombi yao yatakubaliwa, watampelekea mapendekezo yao juu ya nini kifanyike kulileta taifa pamoja.

“Tumeomba rasmi kukutana naye kueleza namna vipi mioyo yetu hatukusudii kumzingua, nasi hatutegemei kuzinguliwa kwani hatuko kwenye biashara ya siasa. Bali tunataka mustakabali utakaorejesha furaha haki na ustawi wa jamii.

“Tunategemea kumkabidhi mapendekezo  ya kina nnamna ya kuanza ukurasa mpya wa sissa uchumi kijamii ns kuleta utengamano wa Taifa,” amesema Mbowe.

error: Content is protected !!