May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema kuanza operesheni nchi nzima

Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kinakusudia kuanza operesheni nchi nzima. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na Watanzania kupitia mitandao ya kijamii leo tarehe 11 Aprili 2021, Mbowe amesema, chama hicho kitafanya operesheni ili wananchi wajue hatma ya nchi yao.

“Chama chetu kitaanza operesheni maalumu ili Watanzania wajue hatma ya nchi yao, kwasababu za kimkakati na kiuslama itoshe kuishia hapo.

“Wanachama wetu popote walipo wajiandae, tunataka kukipekea chama katika viwango viya vya kitaifa na kimataifa, sisi sio watu wa kukatishwa tamaa,” amesema Mbowe.

Akiongozwa na kauli ya kamwe, kamwe isijirudie (utawala wa Rais John Magufuli), Mbowe amesema mpango wa kuzunguka nchi nzima, uliwekwa na chama hicho tangu Januari mwaka huu, na kwamba wakati wanajiweka sawa ‘Magufuli (Rais Magufuli), akatangulia mbele ya haki.’

Amesema, kutokana na hilo (Rais Magufuli kufariki dunia), chama hicho kinajipanga tena na namna ya kuanza kuzunguka nchi nzima, awali operesheni hiyo amesema ilipaswa kuanza mwezi huu (Aprili).

Kiongozi huyo amesema, suala la kusimamia demokrasia ya nchi, sio la wanasiasa pekee, na kwamba ni ulegevu wa wananchi umelifikisha Taifa kufika hapa lilipo.

“Tumefika hapa kwa kuwa tumekuwa legelege, ni jukumu letu wote kusimamia demokrasia,” amesema Mbowe huku akisistiza uhitaji wa Katiba Mpya si suala la hiyari ya watawala.

“Uhitaji wa Katiba Mpya hauhitaji kuwa utashi wa rais na chama chake. Katiba ni msingi, ni roho ya Taifa. Uhitaji wa Katiba Mpya haupaswi kuwa kwa rais ama chama chake.

“Hatuhitaji mjadala wa kuwa na Katiba, mjadala umeishafungwa, na ndio maana tulianza mchakato wa Katiba,” amesema Mbowe.

error: Content is protected !!