Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Kinyaiya: Rais Samia ana busara
Habari za Siasa

Askofu Kinyaiya: Rais Samia ana busara

Spread the love

 

ASKOFU Mkuu, Jimbo Kuu la Katoliki Dodoma, Beatus Kinyaiya, amemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kwamba ni kiongozi shupavu, mkakamavu, jasiri, mtenda haki, mwenye hekima na busara. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

“Rais huyu ni shupavu, mkakamavu, jasiri, mtenda haki, mwenye hekima na busara. Hii ni bahati kwa Tanzania kuwa na rais mwanamke katika Ukanda wa Afrika Mashariki,” amesema Askofu Kinnyaiya.

Askofu Kinyaiya ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Aprili 2021, wakati akizungumza kwenye ibada maalumu ya wamama wakatoliki Tanzania (WAWATA).

Katika mahubiri yake, amesema Mungu amempa heshima kubwa mwanamke kwa kuzingatia mambo mbalimbali.

Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Amesema, vigezo ambavyo Mungu aliviangalia kwa mwanamke ni pamoja na uaminifu, upendo, uthamini, utendaji wa kazi na nafasi ya mwanamke katika jamii.

Askofu Kinyaiya amesema, kwa kuzingatia vigezo hivyo, Mungu alimfanya mwanamke kuwa muhimu na ndiyo maana hata wakati wa siku ya kufufuka kwa Yesu, aliyetokewa wa kwanza na kupata habari alikuwa mwanamke.

Kiongozi huyo wa kiroho amesema, mwanamke anayo heshima ya kuheshimiwa na kusikilizwa, kwa kuwa Mungu kamthamini kwa kiwango cha juu.

Kutokana na hali hiyo, Askofu Kinyaiya amekemea watu wenye tabia ya kunyanysa wanawake, hasa wanaodhani wamewanunua wake zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!