Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aanza kufukua makaburi
Habari za Siasa

Zitto aanza kufukua makaburi

Spread the love

 

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema, Taifa linalipa gharama ya kuendesha nchi gizani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Zitto ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Aprili 2021, wakati akizungumzia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2019/2020, jijini Dar es Salaam.

“Tunalipia gharama ya kuendesha nchi gizani, tusingekuwa tumeminya misingi ya demokrasia, uhuru wa habari, kuvunja taaisi za uwajibikaji, bunge na kamati zake. 

“…kwa hakika haya ambayo Charles (CAG – Charles Kichere) aliyoyaeleza, tungekuwa na ahueni, lakini taarifa hii imeonekana ni nzito sana kwa sababu tulikuwa gizani, tunalipia gharama ya kuendesha nchi gizani,” amesema Zitto

Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma Mjini, ameishauri serikali kupitia Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu wa miradi ya kimkakati, kwa madai kwamba ina harufu ya ufisadi.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ufufuaji Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere (Sigle’s Gorge).

Kuhusu ATCL, Zitto ameishauri serikali kupitia Ofisi ya CAG, kufanya ukaguzi maalumu wa fedha Sh. 1 Trilioni, zilizotumika kununua ndege pamoja na usimamizi wa mkataba wa ukodishwaji ndege hizo kati ya Wakala wa Ndege za Serikali na ATCL.

“Jambo hili ni muhimu sana, kwa sababu uzoefu unaonesha kuwa, kila jambo lenye harufu ya wizi au matumizi yenye mashaka basi serikali huliamishia jambo hilo ikulu (Kwa kuwa inajua ukaguzi wake hautawekwa wazi).

 

“Hata kwenye fedha Shilingi 1.5 trilioni ambazo tulizianisha kuwa hazijulikani ziliko kutokana na uchambuzi wetu wa Ripoti ya CAG ya mwaka 2016/17, baada ya kuibana serikali na kumtaka CAG afanye uchunguzi maalum, mwishowe serikali ilihamishia Ikulu matumizi ya Shilingi 976 bilioni kati ya hizo shilingi 1.5 trilioni ili isihojiwe,” amesema Zitto.

Sambamba na hilo, amehoji shirika hilo liliwezaje kurudisha gawio serikalini, wakati lilijiendesha kwa hasara katika kipindi cha miaka mitano mfululizo?

“CAG hakueleza katika Ripoti yake ilikuwaje shirika ambalo lina hasara kiasi hiki, licha ya ruzuku ya serikali, liliweza kulipa gawio kwa serikali?

“Ilikuwa ni usanii! katika uchambuzi wa Ripoti ya CAG Mwaka 2017/18 tulisema haya kuhusu ukaguzi wa ATCL,” amesema Zitto.

Amesema, pamoja na ATCL kununua ndege, kwa miaka mitano (2015/16 -2019/20), limekuwa likitengeneza hasara ya jumla ya Sh. 153 bilioni, ikiwemo hasara ya Sh. 60.25 bilioni kwa mwaka 2019/2020.

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

“Serikali imeisaidia kampuni ya ndege kiasi cha Sh. 153.711 Bilioni kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na maendeleo.

“Fedha hizi za walipakodi, serikali imekuwa ikizitoa kama ruzuku kwa ATCL. Hata hivyo, shirika limekuwa na hasara ya jumla ya shilingi 153 bilioni katika miaka mitano,” amesema Zitto.

Akizungumzia ujenzi wa reli (SGR), Zitto amesema Ripoti ya CAG imebainisha, kwamba mradi huo umechelewa kukamilika huku ukiwa na dosari kadhaa, ikiwemo kutojengwa kwa kipande cha reli urefu wa kilometa tatu, kinyume na matakwa ya mkataba.

Kutokana na dosari hizo, Zitto amependekeza CAG kufanya ukaguzi maalumu wa manunuzi ya mradi huo ili kubaini kama fedha zilizotumika zina thamani sawa na mradi huo.

“Hivyo mapendekezo yetu ya kwanza ni kwa CAG kufanya ukaguzi maalumu wa manunuzi ya mradi huu na kulinganisha kama ungetekelezwa tofauti, ili kutambua kama ni mradi wenye thamani ya fedha (value for money) na namna gani ya kumalizia kuutekeleza kwa ufanisi zaidi,” ameshauri Zitto.

Akizungumzia mradi wa kufua umeme wa Stigler’s Gorge, Zitto amesema, CAG amebainisha hoja nzito ambazo zinaonesha, mradi huo unaogharimu Sh. trilioni sita, unatekelezwa kiholela.

“Mkataba huu wa TANESCO na TANROADS haukuidhinishwa na Bodi ya TANESCO. Madhara ya mfumo huu wa utekelezaji wa mradi ni usimamizi mbovu wa mradi ambao ulisababisha kingo za bwawa kubomoka na kusababisha mafuriko makubwa sana,” amedai Zitto.

Akizungumzia hasara inayotokana na mradi wa bomba la gesi Mtwara unalosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), amesema tayari Tanzania inaelea kwenye hasara.

“Ni vema kuwakumbusha Watanzania kuwa, CAG pia katika taarifa ya mwaka huu ameonesha kuwa TPDC lina mtaji hasi wa Shilingi Bilioni 332 ambao

umesababishwa na mkopo ambao serikali yetu ilichukua kutoka China Kwa ajili ya Ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam.

“Mkopo ule ni wa thamani ya Shilingi Trilioni 3.23. TPDC wameshindwa kulipa mkopo huu kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kuachana na mkakati wa kuzalisha umeme kwa Gesi Asilia, na badala yake kuwekeza kwenye Mradi wa Umeme wa

Bwawa la Mwalimu Nyerere,” amesema.

Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG ya Mwaka 2015/16 Bomba la Gesi lenye uwezo wa

Ameshauru serikali itazame upya masuala ya utawala bora katika usimamizi wa miradi mikubwa kwa kuondokana na uholela unaoendelea sasa.

“Fedha nyingi zimekwishaingizwa katika miradi hii, hivyo ni lazima kuimaliza. Hata hivyo ni muhimu kurekebisha makosa yote ambayo CAG ameyaonesha katika taarifa yake.

“Tunapendekeza pia serikali iiache TPDC lifanye kazi yake kibiashara na kurudi katika mpango kabambe wa kuzalisha na kusambaza umeme, ili uwekezaji uliofanywa katika Bomba la Gesi, uwe na manufaa kwa Taifa letu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!