Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Chato maandalizi ya kumuaga JPM yashika kasi
Habari Mchanganyiko

Chato maandalizi ya kumuaga JPM yashika kasi

Spread the love

 

UWANJA wa mpira wa Chato, Geita ambao utatumika katika shughuli ya kuaga mwili ya Hayati John Magufuli, upo kwenye maandalizi. Anaripoti Tunu Herman, Chato … (endelea).

Rais Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Mchi 2021, jijini Dar es Salaam kwa ugionjwa wa moyo.

Serikali wilayani Chato inatumia magreda pamoja na vifaa mbalimbali vya kisasa, kuhakikisha maandalizi hayo yanakamilika haraka.

Mwandishi wetu aliyepo Chato, anaeleza kutawala kwa utulivu huku mijadala ya hapa na pale ikiendelea kuhusu kifo cha Rais Magufuli.

Tayari uwanja huo umebadilika mandhari yake na kuwa ya kuvutia.

Morine Tambwe, mmoja wa wakazi wa Chato anasema, wilaya hiyo imeumizwa na kifo hicho.

“Hapa tumeumia zaidi kwa kuwa, ndio kiongozi pekee aliyeiweka Chato kwenye taswira ya Tanzania na kujulikana,” amesema.

Amesema, vijana wa Chato walikuwa na matumaini makubwa kuendelea kubaki ndani ya wilaya hiyo kutokana mabadiliko yaliyodhihirika kwa kasi ya pekee.

“Tunaamini viongozi wanaomfuata, hawataitelekeza Chato na maeneo mengine,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

error: Content is protected !!