Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa amwaga chozi mbele ya mwili wa Dk Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Majaliwa amwaga chozi mbele ya mwili wa Dk Magufuli

Majaliwa Kassim, Waziri Mkuu wa Tanzania akiaga mwili wa Hayati John Magufuli
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amejikuta akibubujikwa machozi, mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Dk. John Pombe Magufuli. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Majaliwa akiwa ameongozana na mkewe, Mary mara baada ya kufika mbele ya mwili wa Dk. Magufuli, Majaliwa alisimama kutoa heshima za mwisho, kasha akatoa kitambaa chake na kuanza kujifuta machozi.

Mara baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho, Majaliwa aliondoka.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiaga mwili wa Hayati John Magufuli

Shughuli ya kuaga imeongozwa na Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya viongozi wengine waliotoa heshima za mwisho ni; Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Bashiru Ally, Spika Mstaafu Anne Makinda, Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Sulieman Abdulla.

Pia, Mama Maria Nyerere, Mjane wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wengine ni, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Naibu wake upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu, mawaziri na naibu mawaziri, katibu wakuu na naibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya, wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali na siasa.

Mwili wa Hayati Magufuli utaagwa rajiwa kuagwa Dar es Salaam kwa siku mbili (Jumamosi na Jumapili), kisha tarehe 22 Machi 2021, mwili huo utaagwa katika Makao Makuu ya Nchi Dodoma.

Tarehe 23 Machi 2021, mwili wa Hayati Rais Magufuli utaagwa visiwani Zanzibar, kisha utasafirishwa Mwanza kwa ajili ya shughuli ya kuuaga tarehe 24 Machi 2021.

Baada ya kuagwa Mwanza, mwili wa Hayati Rais Magufuli utaagwa na wananchi wa Chato mkoani Geita, tarehe 25 Machi mwaka huu.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!