May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Ruwa’ichi: Magufuli alikuwa mpenda haki

Spread the love

 

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Juda Thadeus Ruwa’ichi, amemzungumzia Hayati Rais John Pombe Magufuli, akisema alikuwa ni mtu mwenye imani na mpenda haki. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Askofu Ruwa’ichi amesema hayo leo Jumamosi tarehe 20 Machi 2021, katika Misa Takatifu ya kuuaga mwili wa Hayati Magufuli (61), iliyofanyika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam.

Hayati Rais Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021 katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, kwa matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.

Na mwili wake unatarajiwa kuzikwa Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, kijijini kwao Chato mkoani Geita.

“Hayati Magufuli alikuwa mtu wa imani na mtu wa haki, alimpa Mungu yale yaliyompasa kama kiumbe wake na aliwapa wengine mastahiki yao na pia akajipa mwenyewe yale ambayo ni mastahili yake kama kiumbe wa Mungu,” amesema Askofu Ruwa’ichi

Mkuu huyo wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, amewaomba Watanzania kumuombea Hayati Magufuli.

“Na kwa sababu hiyo, tunayo kila sababu ya kuamini kwamba anastahili kuombewa kusudi Mungu baba wa huruma amsamehe katika chochote tulichopungua katika majitoleo, uwajibikaji na utendaji wote kwa huruma yake amjaalie pumziko la milele,” ameomba Askofu Ruwa’Ichi.

Amewaomba Watanzania kumuamini Mungu na kuliombea Taifa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

“Taifa limeingia kwenye msiba mzito wa kuondokewa na rais wetu Magufuli, tuko kwenye majonzi na maombolezo hata hivyo tunapoombeleza tutie nguvu na imani yetu. Imani yetu katika Kristo ambaye Hayati Magufuli alimuamini, alimfuata alimshuhudia na kumtumikia,” amesema Askofu Ruwa’ichi.

“Tunapomuombea Hayati John Magufuli napenda kuwaalika tuliombee pia Taifa hili ambalo alilipenda na alilihudumia kwa nguvu zake zote kusudi taifa letu liendelee kuwa na umoja, amani liendelee na utawala wa haki, liendelee kujituma katika ksuhughulikia usawa utu na maendeleo ya raia wake wote,” amehimiza Askofu Ruwa’ichi.

Janeth Magufuli, mke wa Hayati John Magufuli

Akizungumzia majukumu mapya ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Askofu Ruwa’Ichi amesema kuwa rais wa nchi sio kazi rahisi kwani ni jukumu zito ambalo linabebesha wajibu wa kuwahudumia kwa usawa raia wote.

Kifuatia jukumu hilo zito, Askofu Ruwa’Ichi amewaomba Watanzania kumuombea Rais Samia.

“Najua kwamba Mama Samia alishirikiana kwa karibu na hayati Magufuli wakati akiwa makamu wake kwa hiyo hatuna wasiwasi kwamba anaielewa nchi, anaifahamu nchi, anajua vipaumbele vyake na anaendeleza kwa juhudi yale yote mema ambayo yalishughulikiwa na Hayati Magufuli.’’

Rais John Magufuli

‘’Kwa kuwa nimesema jukumu la kuongoza nchi ni zito nawaalikeni kumuweka katika sala, mumpe ushirikiano na kusiamamana nae katika kutafuta ustawi na manedeleo katika kila namna kwenye nchi hii,” amesema Askofu Ruwa’ichi.

Misa hiyo imehudhuliwa na viongozi wa kisiasa na kiserikali mbalimbali akiwemo, Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

error: Content is protected !!