Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Chalamila ‘akomalia’ daladala Mbeya
Habari za Siasa

RC Chalamila ‘akomalia’ daladala Mbeya

Spread the love

 

ALBER Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema, serikali haitaondoa bajaji wala pikipiki (bodaboda), kufanya biashara ya kusafirisha abiria katika barabara kuu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya…(endelea).

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 15 Machi 2021, baada ya asubuhi ya leo, kutokea mgomo wa daladala wakitaka bajaji na bodaboda kupigwa marufuku kusafirisha abiria kupitia barabara kuu ya Uyole- Mbalizi na Uyole- Soko Matola

“Hatuziondoi Bajaji ,” amesema Chalamila akisisitiza kwamba, endapo daladala zitaendelea kugoma, basi ataagiza mabasi ya serikali ikiwa ni pamoja na magereza, polisi na mahakama kubeba abiria hasa wanafunzi.

Chalamila amasema, bajaji na pikipiki wataendelea kutumia barabara hiyo, kwa sababu ni haki yao na wanalipa kodi kama wengine.

Kwenye vituo vya daladala cha Kabwe, Mbeya leo kulikuwa na idadi kubwa ya abiria baada ya daladala kugoma.

Daladala walichukua hatua hiyo kwa madai, bajaji na pikipiki zinavuruga biashara hiyo na hivyo kushinikiza kuondolewa barabara kuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!