Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Tangulizi NEC yamteua diwani NCCR-Mageuzi
Tangulizi

NEC yamteua diwani NCCR-Mageuzi

Spread the love

 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), imemteua Renatha Lihange Mizungo, kuwa Diwani Viti Maalumu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Kigoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Alhamisi tarehe 18 Februari 2021 na Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk. Wilson Mahera.

Kwenye taarifa hiyo, Dk. Mahera amesema, uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa, baada ya Chama cha NCCR-Mageuzi kupata madiwani wawili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Kigoma kwenye Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

“Kifungu cha 35(1) (C) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287 kifungu cha 19 (1) (C) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), sura ya 288 pamoja na kifungu cha 86A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, sura ya 292 vinaweka takwa la kuwa na madiwani wanawake wa viti maalumu wasiopungua theluthi moja ya wajumbe wote wa halmashauri husika,” imesema taarifa ya Dk. Mahera.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera

Taarifa ya Dk. Mahera imesema “hivyo, NEC hufanya uteuzi wa madiwani wanawake wa viti maalumu katika halmashauri zote nchini.”

“Kwa kuzingatia ushindi wa chama husika, katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, NCCR-Mageuzi katika Halmashauriya Kasulu kilipata madiwani wawili,” imeeleza taarifa hiyo.

Mkurugenzi huyo wa uchaguzi NEC, amesema uteuzi huo umefanyika baada ya tume hiyo kupokea barua ya utambulisho wa Mizungo, kutoka kwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi.

“Baada ya kupokea fomu namba 8E kutoka kwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, iliyowasilishwa kwa barua yenye Kumb. Na. NCCR-M/MM/TV/15/125 ya tarehe 5 Februari 2021, tume katika kikao chake cha tarehe 17 Februari 2021 ilipitia na kukagua fomu hiyo,” imesema taarifa ya Dk. Mahera na kuongeza.

“Na baada ya kujiridhisha imemtea ndugu Renatha Lihange Mizungo kuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauyri ya Wilaya ya Kasulu kupitia chama cha NCCR-Mageuzi.”

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!