Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Taifa Stars imeshindwa kuendelea, ilipoishia
Makala & UchambuziMichezoTangulizi

Taifa Stars imeshindwa kuendelea, ilipoishia

Spread the love

 

MARA baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwenye hatua ya makundi, timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kuendelea pale ilipoishia wakati waliposhiriki michuano hiyo mwaka 2009. Anaandika Kelvin Mwaipung, Dar es Salaam … (endelea).

Katika michuano hiyo ya mwaka 2009, iliyofanyika nchini Ivory Coast ilishirikisha timu nane tu, huku Stars ikiwa chini ya Kocha raia wa Brazil, Marcio Maximo ilipangwa kundi A, sambamba na timu za Zambia, Senegal pamoja na wenyeji wa michuano.

Mara baada ya kukamilika hatua ya makundi Taifa Stars ilijikuta ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne na kushindwa kusonga kwenye hatua inayofuata ya robo fainali mara baada kulazimisha sare ya bao 1-1 na Zambia.

Miaka 12 baadaye Taifa Stars inacheza tena michuano hiyo huku matumaini yakiwa ni kufanya vizuri kwa kuwa siyo wageni tena wa michuano hiyo, lakini inajikuta inarudia tena ilichokifanya 2009 kwa kuondoshwa kwenye michuano hiyo katika hatua ya makundi.

Etienne Ndayiragije, Kocha wa Taifa Stars

Hakuna hatua yoyote iliyoonekana kupigwa kama 2009 ilimaliza kwenye nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne baada ya kushinda mchezo mmoja, kupoteza mmoja na kwenda sare moja, hakuna tofauti na timu hiyo ilichokifanya kwenye michuano ya Chan mwaka huu nchini Cameroon.

Huenda mategemeo ya watanzania wengi kuona wanafika nchi ya ahadi kwenye maendeleo ya mpira wa miguu hayapo kwenye kizazi hiki cha sasa kama tunavyoamini na kusubiri, kinachokatisha tamaa zaidi ni hizi nchi kama Cape Cerde ambao walionekana kuwa chini kisoka lakini kwa sasa hawakamatiki.

Labda tunaweza tukawa hatujachelewa sana kama mipango thabiti itawekwa kwa hizi timu za vijana chini ya umri wa miaka 10 na 20 ambazo zote zimefuzu kwenye michuano ya AFCON kwa ngazi zao na kuhakikisha vizazi hivi havipotei ili kuondoa kisingizio cha kuwa hatuna uzoefu.

Labda tunahitaji kuwa na vijana wengi kariba ya Kelvin John ambao wanacheza nje ya nchi, angalau hata baada ya miaka mitano ikiitwa timu ya Taifa tuwe na wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa kucheza soka hasa barani Ulaya.

Kwa sasa hatujui nani wa kumlaumu, wengine wameenda mbali kutaka kocha, Ettiene Ndayilagije afukuzwe, hii haiwezi kuwa mwarobaini wa matatizo yetu kwa kuwa miezi 13 iliyopita tulimuondoa Kocha, Emmanuel Amunike ambaye alifanikisha Stars kufuzu AFCON lakini bado timu imeenda CHAN na imeharibu tena.

Hichi kivuri cha kukosa uzoefu tunachokitumia kwa sasa ipo siku kitaondoka na watu watajua ukweli ya kwamba tunataka kupita njia fupi kwenye maendeleo ya mpira wa miguu huku tukifahamu ya kuwa haiwezekani.

Ni wakati sasa wa mamlaka za soka kuchukua uamuzi mgumu ili kuondoa sababu hizi za kusema tunakosa uzoefu ili Stars iweze kufanya vizuri katika michuano inayokuja kwa kuendelea pale ilipoishia kama itafanikiwa kufuzu tena kwenye michuano ya AFCON au CHAN.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

error: Content is protected !!