May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha TP Mazembe avutiwa na kiungo wa Simba

Felix Mwamba, Kocha wa TP Mazembe

Spread the love

 

KOCHA wa kikosi cha TP Mazembe, Felix Mwamba ameonekana kuvutiwa na kiwango cha kiungo wa klabu ya Simba Laary Bwalya mara baada ya kuonesha kutamani kumtumia kwenye kikosi chake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mazembe ambao wapo nchini Tanzania na siku ya kesho watashuka dimbani kumenyana na Simba kwenye michuano ya Simba Super Cup katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, majira ya saa 11 jioni.

Akijibu swali la mwandishi wa habari juu ya mchezaji gani kutoka upande wa klabu ya Simba anayemvutia kocha huyo akusita kusema kuwa “Ningekuwa naweza kumchukua mchezaji mmoja kutoka Simba ningechukua Bwalya”

Bwalya ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea klabu ameonesha kiwango kikubwa hasa kwenye michuano ya kimataifa hasa kwenye michezo miwili ya nyumbani na ugenini dhidi ya FC Platinum.

error: Content is protected !!