Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Bobi Wine apinga matokeo, ajiita rais mteule
Kimataifa

Bobi Wine apinga matokeo, ajiita rais mteule

Robert Kyagulanyi 'Bobi Wine', akipiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Uganda
Spread the love

ROBERT Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, amepinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda mpaka sasa akidai hila zimefanyika. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 15 Januari 2021, Bobi Wine amesema, uchaguzi huo umetawaliwa na wizi wa kura huku akimtuhumu mpinzani wake ambaye ni rais wan chi hiyo, Yoweri Museveni kwamba, ameshiriki kuhujumu uchaguzi huo.

Kutokana na kudai kuwepo kwa wizi huo, ‘amejitangaza’ kuwa rais mteule wa Uganda. Mpaka sasa Museveni anaonga kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura zote zilizohesabiwa.

Bobi Wine amesema, Taifa la Uganda limeshuhudia wizi mkubwa wa kura kuwahi kutokea, lakini hata hivyo hajaweka ushahidi wake wazi.

Pia amesema, hatua ya serikali kuzima intaneti imechangia kwa kaisi kikubwa kuvuruga matokeo ya uchaguzi huo huku akidai, mawakala wake wamekuwa wakikamatwa kwenye vituo vya kura.

Simon Byabakama, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amemtaka Bobi Wine kuweka ushahidi wake hadharani juu ya madai yake ya wizi wa kura.

Amesema kuwa wagombea walikuwa na mawakala ambao walishuhudia kuhesabiwa kwa kura katika vituo vya kukusanya na kuhesabu kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!