Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Taswira ya matokeo kidato cha nne 2020  
ElimuTangulizi

Taswira ya matokeo kidato cha nne 2020  

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde
Spread the love

BARAZA Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya mthani wa kidato cha nne, uliofanyika mwaka 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Matokeo hayo, yametangazwa leo Ijumaa tarehe 15 Januari 2021 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde jijini Dar es Salaam.

“Jumla ya watahiniwa wa shule 373,958 sawa na asilimia 85.84 ya watahiniwa 434,654 wenye matokeo ya kidato cha nne wamefaulu,” amesema Dk. Msonde.

Amesema, wasichana waliofaulu ni 193,672 sawa na asilimia 85.44 na wavulana ni 180,286 sawa na asilimia 86.27.

Dk. Msonde amesema, mwaka 2019, watahiniwa 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo.

“Hivyo, ufaulu wa watahiniwa wa shule umeongezeka kwa asilimia 5.19 ikilinganishwa na mwaka 2019,” amesema Dk. Msonde.

Akifafanua ubora wa ufaulu, Dk. Msonde amesema, uora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya kwanza hadi tatu wakiwa 152,909 sawa na asilimia 35.10 wakiwemo wasichana 66,899 (29.51%) na wavulana 86,010 (41.17%).

“Mwaka 2019 watahiniwa waliopata ufaulu wa madaraja I – III walikuwa 135,301 sawa na asilimia 32.01. Hivyo, ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.09,” amesema Dk. Msonde

Katibu mtendaji huyo amesema, takwimu za matokeo zinaonesha watahiniwa wamefanya vizuri zaidi masomo ya msingi ambapo ufaulu wa masomo hayo uko juu ya wastani kati ya asilimia 50.53 na 94.83.

Aidha, amesema, takwimu za matokeo zinaonesha watahiniwa hawakufanya vizuri katika masomo mawili (02) ya Fizikia na Hisabati, japokuwa katika somo la Fizikia ufaulu umeendelea kuimarika kutoka asilimia 48.38 kwa mwaka 2019 hadi asilimia 48.87 kwa mwaka 2020.

Katika mtihani huo, Paul Luziga wa Shule ya Sekpndari Pandahill ya jijini Mbeya, amewaongoza wenzake kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa.

Fuatilia hapa chini mpangilio wa wengine tisa kwenye kundi hilo la wanafunzi 10 bora kitaifa, lakini mchanganuo wa wasichana na wavulana kumi bora.

Dk. Msonde amesema, takwimu za matokeo zinaonesha mpangilio wa shule, mikoa na halmashauri zilizofanya vizuri, kuongeza au kupunguza ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo ni kama ilivyoainishwa hapa chini;

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!