Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa akagua ujenzi daraja la JPM, MV Mwanza
Habari za Siasa

Majaliwa akagua ujenzi daraja la JPM, MV Mwanza

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa daraja la JPM lenye urefu wa kilomita 3.2 linalojengwa ziwa Victoria kwa gharama ya Sh.699 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Daraja hilo linajengwa kwa lengo la kuunganisha barabara kuu ya Usagara-Sengerema litakapokamilika litakuwa la kwanza kwa urefu katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki.

Pia, Majaliwa amekagua ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu unaogharimu Sh.89.76 bilioni ambao hadi sasa umefikia asilimia 70 kwa ujumla wake.

Waziri Mkuu amekagua miradi hiyo ya kimkakati leo Ijumaa, 18 Desemba, 2020 akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Mradi hiyo yote inajengwa kwa kutumia fedha za ndani.

Baada ya kukagua miradi hiyo, Majaliwa amesema, ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake na kwamba ujenzi huo ni mfululizo wa ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji nchini.

“Ujenzi wa miradi hii utarahisisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi kwa sababu huwezi kupata maendeleo ya watu bila kujenga vitu. Wananchi endeleeni kuiamini Serikali yenu.”

Waziri mkuu, Majaliwa amesema, hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi hiyo ni ya kujivunia kwa sababu itakapokamilika itawawezesha wananchi kusafiri na kusafirisha mizigo
yao kwa urahisi.

Kuhusu ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi, Majaloiwa amesema, tayari mradi huo umeshaanza kunufaisha kwani Watanzania zaidi ya 370 wameajiriwa katika mradi huo.

Waziri Mkuu amesema tayari daraja hilo limepewa jina la Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili iwe kumbukumbu kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuboresha maendeleo nchini.

Ujenzi wa daraja la JPM unaojengwa na kampuni ya M/S China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ulianza Februari 2020 na unatarajiwa kukamilika Februari 2024.

Ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu unatekelezwa na kampuni ya GAS Entec na Kampuni ya KANGNAM Corporation zote za Korea Kusini zikishirikiana na SUMA JKT.

Meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu inayotarajiwa kukamilika Desemba 2021 itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari makubwa matatu na madogo 20.

Wakizungumzia kuhusu ujenzi wa miradi hiyo Wabunge wa Mkoa wa Mwanza walimpongeza Rais Magufuli kwa kuwa miradi hiyo inakwenda kuboresha maendeleo ya mkoa wao.

Mbunge wa Misungwi, Alexanda Mnyeti amesema ujenzi wa mradi ya daraja la JPM ni wa ajabu na hakuna aliyefikiria kama utatekelezeka. “Mradi huu ni wa muujiza tunamshukuru sana Rais.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!