Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Morrison atemwa Simba
Michezo

Morrison atemwa Simba

Spread the love

WINGA raia wa Ghana anayekipiga klabu ya Simba, Bernard Morrison ameachwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 kilichosafiri kwenda Harare Zimbabwe kucheza mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya FC Platinum. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikosi hicho kimeondoka leo Ijumaa tarehe 18 Desemba 2020 majira ya saa 4:30 asubuhi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) huku kukiwa hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusu kuachwa kwa Morrison.

Ni mara ya pili kwa Morrison kuwekwa pembeni kwenye kikosi cha Simba kinaposafiri kwenye michezo ya ugenini mara baada ya kuachwa kwenye safari ya Mbeya.

Simba ilikwenda Mbeya kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Morrison ambaye alijiunga na Simba akitokea Yanga kwenye dirisha kubwa la usajili, ameonekana kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Simba tofauti na mategemeo ya wengi kutokana na ubora aliouonesha akiwa na Yanga.

Kikosi kamili cha Simba kilichosafiri kuelekea Zimbabwe kuchuana na FC Platinum tarehe 23 Desemba 2020, ni makipa Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ally Salim, huku mabeki wakiwa Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Pascal Wawa, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Gadiel Michael na Josh Onyango.

Kwa upande wa viungo ni; Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Rally Bwalya, Francis Kahata, Clotous Chama na Taddeo Lwanga.

Washambuliaji wakiongozwa Nahodha wao; John Bocco, Medie Kagere, Chris Mugalu, Miraji Athuman, Luis Miquisone na Ibrahim Ajibu.

Wachezaji wengine walioachwa kwenye kikosi hiko ni beki wa kati Kennedy Juma, Gerson Fraga ambaye ni majeruhi, Charles Ilamfya pamoja na David Kameta (Duchu) ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya vijana kilichopo Saudi Arabia.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!