Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yazungumzia rufaa ya Mdee na wenzake 18
Habari za Siasa

Chadema yazungumzia rufaa ya Mdee na wenzake 18

John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania kimesema, Halima Mdee na wenzake 18 bado hawajawasilisha rufaa zao za kupinga kufukuzwa uanachama wa chama hicho. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Chadema imetoa taarifa hiyo jana Alhamisi tarehe 3 Desemba 2020 ikiwa zimepita siku mbili tangu Mdee na wenzake hao kutangaza kukata rufaa Baraza Kuu kuoinmga uamizi wa kamati kuu wa kuwafukuza.

Mdee na wenzake 18, walifukuzwa Chadema kwa tuhuma za usaliti, kughushi na kujipeleka bungeni kuapishwa tarehe 24 Novemba 2020 na Spika Job Ndugai kuwa wabunge wa viti maalum, wakijua chama hicho, hakijapendekeza majina yao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uamuzi wa kamati kuu, ulitolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe tarehe 27 Novemba 2020 akisema, Mdee na wenzake wamekisaliti chama na kama hawaridhiki na uamuzi huo wa kuwafukuza, wanaweza kukata rufaa baraza kuu ndani ya siku 30 au kuomba radhi.

Tarehe 1 Desemba 2020, Mdee na wenzake 18 wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, walisema hawana lengo la kuondoka ndani ya chama hicho na watabaki kama ‘wanachama wa hiari’ wakati mchakato wa kukara rufaa ukiendelea.

Jana Alhamisi, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema, wamesikia kilichosemwa na waliokuwa wanachama wao Mdee na wenzake wanaokusudia kukata rufaa.

Mrema amesema, sababu ya Mdee na wenzake ya kutofika mbele ya kamati kuu kama walivyoita kwa kigezo kwamba wangeweza kufanyiwa fujo haina msingi.

Alisema, ili kuhakikisha usalama wao, kikao hicho kilichokuwa kimepangwa kifanyikie makao makuu ya chama hicho Kinondoni, Dar es Salaam, kilihamishiwa hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach “ili wawe huru kufika na kujieleza mbele ya kikao kikao cha kamati kuu.”

“Kwa maana hiyo, suala hilo limetumika tu kama kisingizio dhidi ya uamuzi wao wa kukwepa kuja kujitetea mbele ya kikao cha kamati kuu,” alisema Mrema.

Mrema alisema, “pamoja na nia yao ya kukata rufaa, mpaka sasa (jana jioni) chama hakijapokea rufaa yoyote.”

“Izingatiwe uamuzi wa kuwavua nafasi zao za uongozi ndani ya chama na kuwafukuza uanachama unaendelea kutamalaki na unapaswa kuzingatiwa na wanachama wote na mamlaka zote hadi hapo utakapobatilishwa na baraza kuu iwapo wahusika wakikata rufaa na rufaa yao kukubaliwa,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!