Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba yasajili mbadala wa Fraga
Michezo

Simba yasajili mbadala wa Fraga

Haji Manara
Spread the love

KLABU ya Simba imefanikiwa kumsaini kiungo makabaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda, Taddeo Lwanga ambaye amekuja kuziba pengo la Gerson Fraga ambaye amepata jeraha la goti litakalomweka nje kwa muda mrefu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Mchezaji huyo anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi hiko katika michuano ya kimataifa kwa msimu wa 2020/21 akitokea klabu ya Tanta inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri.

Simba inafanya usajili huo mara baada ya kuruhusiwa na Shirikisho la Mpira Miguu Tanzania (TFF) kuongeza wachezaji 10 huku watano kati ya hao wakiwa wazawa katika kuongeza nguvu kwenye michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika kwa maelekezo ya Shirikisho la Mpira Afrika (CAF).

Hivi karibuni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohamed Dewji alisema kuwa walipeleka maombi TFF yakusajili wachezaji 10 ambao watawasaidia kwenye mashindano ya kimataifa mara baada ya CAF kuruhusu kufanya hivyo kwa klabu zote shiriki.

Simba wamemtangaza mchezaji huyo leo ambaye anakuja kuongeza nguvu kwenye eneo la chini la kiungo mara baada ya kuumia, Gerson Fraga ambaye atakaa nje ya Uwanja kwa miezi sita mara baada ya kupata jeraha kwenye goti.

Mchezaji huyo hatoruhusiwa kucheza kwenye michezo ya Ligi kutokana na Simba kukamilisha idadi ya wachezaji 10 wa kigeni kwenye kikosi chao kutokana na matakwa ya kanuni za TFF na serikali.

Lwanga ambaye ni mzaliwa wa Kampala mwenye umri wa miaka 24, alipita kwenye klabu za Express FC, Sports Club Villa na Vipers FC ya nchini Uganda.

Pia mchezaji huyo amehudumu kwenye timu ya Taifa ya Uganda toka 2005 na kufanikiwa kucheza jumla ya michezo 19 ya kirafiki na kimashindano. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!