Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu afikishwa kwa AG, Zitto na Mdee wasakwa
Habari za SiasaTangulizi

Lissu afikishwa kwa AG, Zitto na Mdee wasakwa

Tundu Lissu, Mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, limepeleka jalada la kesi inayomkabili Tundu Lissu, aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika 28 Oktoba 2020 kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema-Bara na wenzake wawili walikamatwa jana jioni Jumatatu tarehe 2 Novemba 2020 Ofisi za Umoja wa Ulaya (EU) jijini Dar es Salaam kisha kuhojiwa na kuachiwa.

Leo Jumanne tarehe 3 Novemba 2020, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema, linawashikilia watuhumiwa 14 akiwemo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa mahojiano zaidi.

Wengine kwenye hao 14 ni; Godbless Lema, aliyekuwa mgombea ubunge Arusha Mjini na Boniface Jacob, aliyekuwa Meya wa manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo

“Watuhumiwa wote wamekamatwa katika maeneo mbalimbali na upelelezi unaendelea na watuhumiwa watatu akiwemo Tundu Lissu wameachiwa kwa dhamana ya Polisi na jalada limepelekwa kwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi,” amesema Mambosasa.

Kamanda huyo wa polisi amewaonya wanasiasa kuacha tabia ya “kuja kufanya fujo maeneo ambayo siyo majimbo yao na hatimaye wafuate sharia ili kupeleka malalamiko yao ya uchaguzi na si kushawishi watu kufanya maandamano haramu, kuhatarisha maisha ya watu na mali zao.”

Kamanda Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Mambosasa amesema, watuhumiwa wengine wanaotafutwa ni Halima Mdee, aliyekuwa mgombea ubunge wa Kawe, Dar es Salaam kupitia Chadema na Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawataka wajisalimishe mara moja ili kuendelea na mahojiano kwa tuhuma zinazowakabili,” amesema Kamanda Mambosasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!