Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Barabara Ruangwa-Kiranjeranje kuwekwa lami
Habari za Siasa

Barabara Ruangwa-Kiranjeranje kuwekwa lami

Spread the love

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, Serikali ya CCM imepanga kujenga barabara ya kutoka Ruangwa hadi Kiranjeranje kwa kiwango cha lami. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 23 Oktoba 2020 wakati akizungumza na wakazi wa vijiji na kata mbalimbali za wilaya ya Ruangwa ambako alipita kumuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais John Pombe Magufuli na madiwani wote wa kata hizo.

Akizungumza na wakazi hao kwa nyakati tofauti, Majaliwa amesema, barabara hiyo imo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM na tayari Sh.1.2 bilioni zimeshatolewa ili kufanya upembuzi yakinifu na usanifu.

Barabara hiyo itawafanya wakazi hao wasilazimike kupitia Nanganga hadi Lindi wanapotaka kwenda Dar es Salaam.

“Barabara ya kutoka Ruangwa – Nanjilinji – Kiranjeranje ina urefu wa km.120. Barabara hii ukiangalia kwenye ilani yetu, utaikuta iko uk.75. Barabara nyingine ni ya kutoka Ngongo – Mandawa – Namichiga yenye urefu wa km 85 na hii ilipatiwa Sh.800 milioni na kazi ya upembuzi yakinifu imekwishakamilika, sasa kazi iliyobaki ni kutafuta fedha na kuanza ujenzi,” amesema.

Katika hatua nyingine, Majaliwa ambaye ni mbunge mteule wa jimbo la Ruangwa, amesema katika kipindi cha miaka mitano, wilaya hiyo imepokea zaidi ya sh. bilioni 100 kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

“Haijawahi kutokea. Tangu wilaya hii ianzishwe mwaka 1995, imekuwa ikipokea fedha za maendeleo kati ya Sh.3 bilioni hadi Sh.4 bilioni tu. Lakini awamu hii tumepokea Sh.49.5 bilioni kwa ajili ya kazi za maendeleo na hivi karibuni Mheshimiwa Magufuli alitoa Sh.59 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nanganga- Ruangwa kwa kiwango cha lami.”

Katika vijiji vyote alivyosimama na kata za Mandawa, Chikundi, Namichiga na Mbekenyera, Majaliwa amewasihi wakazi hao kuwa ifikapo Jumatano ijayo wajitokeze kwa wingi na kupiga kura za ndiyo kwa Dk. Magufuli na madiwani wa CCM.

“Sisi sote ni wana-Ruangwa na kikubwa tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayachagui chama. Kwani tukijenga barabara, si tutatumia wote? Fanyeni maamuzi sahihi kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi na kumpa kura nyingi Dk. John Pombe Joseph Magufuli,” amesisitiza.

Wakati huohuo, Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Ruangwa kwa kumpitisha bila kupingwa wakati akiwania ubunge wa jimbo hilo. Bado anaendelea na ziara yake kwenye jimbo la Ruangwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!