Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Shein: Nimefanikiwa
Habari za Siasa

Dk. Shein: Nimefanikiwa

Dk. Ali Mohamed Shein
Spread the love

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema, anaondoka madarakani huku akifanikiwa kuacha visiwa hivyo (Unguja na Pemba) vikiwa na amani. Anaandika Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Akizungumza wakati wa kuaga watumishi wa serikali aliyokua akiongoza tangu mwaka 2010, amewataka kuendelea kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuendeleza amani hiyo.

“Naondoka madarakani nikiiacha nchi yenye amani. Ninaondoka madarakani huku nikiwa nimeacha milango yangu ya ushauri wazi kwa anayetaka kuja, lakini ajitahadhari sitaki majungu na fitina,” amesema Dk. Shein.

Amesema, katika maisha yake ametumikia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 51 na kwamba, katika utawala wake Zanzibar, amefanikiwa kujenga misingi mizuri ya uongozi, utawala bora, maendeleo.

“Namaliza muda wa utumishi wangu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano kwa muda wa miaka 51, nikiwa nimefanikiwa kujenga misingi mizuri ya utawala bora, naondoka nikiacha amani na utulivu vimetawala.

“Ninaondoka madarakani huku nikiwa nimepata mafanikio makubwa katika utendaji wa utumishi wa serikali ikiwamo kufanya marekebisho ya sheria katika Baraza la Wawakilishi zipatazo 128,” amesema.

Pia amempongeza Rais John Magufuli kwa kufanyakazi naye kazi kwa ushirikiano na kuwa, (Rais Magufuli) ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kubuni mambo yenye maslahi makubwa kwa Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!