Sunday , 2 April 2023
Home Kitengo Michezo Yanga vs Simba kuchezwa Uwanja wa Uhuru
Michezo

Yanga vs Simba kuchezwa Uwanja wa Uhuru

Spread the love

MCHEZO wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya Simba rasmi utachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungiwa kwa Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya matengenezo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo uliopangwa kuchezwa tarehe  7 Novemba, 2020 ambapo Yanga ndio atakuwa mwenyeji wa mchezo huo ambao hapo awali ulipangwa kuchezwa kwenye Uwanja huo ambao unachukua idadi ya mashabiki 60,000.

Taarifa kutoka ndani ya Bodi ya Ligi nchini imeleza kuwa michezo yote iliyopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa kwa msimu wa 2020/21 yote imehamishiwa kwenye Uwanja wa Uhuru mpaka pale Uwanja huo utakapofunguliwa.

Uwanja huo ambao unatumika kwa klabu za Simba na Yanga kwenye michezo yao ya nyumbani kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na hata ya kimataifa sasa italazimika kuhamisha michezo yao ya kimashindano kwenye Uwanja Uhuru ambao unachukua idadi ndogo ya mashabiki.

Aidha bodi ya Ligi imeelezea kuwa michezo yote ya Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza iliyopangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma imehamishiwa kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa kwa michezo ya Ligi Kuu na Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa mechi za ligi daraja la kwanza mpaka hapo Uwanja utakapokuwa tayari kwa matumizi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!