Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Fatma Karume: Sijazaliwa mahakamani
Habari Mchanganyiko

Fatma Karume: Sijazaliwa mahakamani

Spread the love

FATMA Karume, mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania amesema, hajazaliwa kwa ajili ya kufanya kazi mahakamani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Fatma ametoa kauli hiyo leo Jumatano  tarehe 23 Septemba 2020 wakati anazungumza na MwanaHALISI Online kuhusu uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Mawakili Tanganyika kuagiza kuondolewa katika orodha ya mawakili wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Kamati hiyo imechukua uamuzi huo baada ya kumtia hatiani kwa tuhuma za kukiuka maadili ya uwakili kwa kuishambulia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Tanzania.

          Soma zaidi:-

Alipoulizwa amejipangaje kuhusu uamuzi huo, Fatma ambaye ni mtoto wa Aman Abeid Karume, Rais mstaafu wa Zanzibar amejibu hajapanga kufanya kitu chochote kwani hakuzaliwa mahakamani wala uwakili.

“Sijapanga kufanya kitu, mimi sijazaliwa mahakamani wala uwakili haini define. Maisha yanaedelea,” ameeleza Fatma.

Kuhusu kukata rufaa juu ya uamuzi huo, Fatma aliyepata kuwa Rais wa TLS kati ya mwaka 2018/19 amesema hana mpango huo.

“Uhalali wa maamuzi si kutokata rufaa. Uhalali wa maamuzi ni maamuzi yenyewe, mantiki yake na ubora wake.”

Fatma aliyehudumu kwenye uwakili kwa zaidi ya miaka 20 amesema “nataka maamuzi hayo yabaki kwenye historia ili miaka 100 kutoka leo Watanzania waelewe tulikuwa na mahakama ya aina gani.”

Fatma Karume

Kwa upande wake Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa TLS amesema Fatma ana nafasi ya kukata rufaa juu ya maamuzi hayo.

Licha ya Fatma Karume, kuondolewa katika orodha ya Mawakili wa TLS, wakili huyo, anayo nafasi ya kufanya shughuli zake za uwakili nje ya mipaka ya Tanzania Bara.

Akifafanua hilo, Wakili Frederick Kihwelo, Mwanachama wa TLS  amesema, Fatma hatoweza kufanya kazi za uwakili upande wa Tanzania Bara, lakini anaweza akaendelea kufanya kazi Zanzibar au nje ya Tanzania bara ambazo atasajiliwa kufanya kazi za uwakili.

Wakili Kihwelo ametoa ufafanuzi huo wakati anazungumza na MwanaHALISI Online.

“Kuhusu wakili kuwekwa katika orodha ya mawakili ina maana kuna database na lazima uwe na namba ya uwakili kwa mujibu wa sheria.”

“Lakini ukiondolewa ina maanisha huwezi kufanya kazi ya uwakili Tanzania bara, anaweza fanya Zanzibar kama mwanachama wa Chama cha Mawakili Zanzibar (ZLS),” amesema Wakili Kihwelo.

Wakili Kihwelo amesema “Fatma anaweza akafanya kazi nje ya nchi kama atasajiliwa katika orodha ya vyama vya mawakili katika nchi husika.”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!