Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wanachama, viongozi 28 ACT-Wazalendo  Z’bar mbaroni
Habari za Siasa

Wanachama, viongozi 28 ACT-Wazalendo  Z’bar mbaroni

Spread the love

VIONGOZI na wanachama 28 wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujeruhi na kuwafanyia fujo wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa  hiyo imetolewa leo Jumatano tarehe 23 Septemba 2020 na, Juma Sadi Khamis, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akizungumza na MwanaHALISI Online.

Kamanda Khamis amesema, watu sita walikamatwa kwa tuhuma za kuchora nyuma za wanachama wa CCM huku 22 wakikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kujeruhi wanachama watatu wa CCM katika Msikiti wa Kandagani visiwani humo.

“Kulikuwa na matukio ya kuchorwa baadhi ya majumba  yanayolengwa ya CCM, baada ya kupata taarifa hiyo, tulifanya operesheni kuanza kuwatafuta wanaohusika, tuliwakamata watu sita na tunaendelea nao na utaratibu wa kesi,” amesema Kamanda Khamis.

Kamanda Khamis amesema “baada ya hilo, ikatokea tukio la kushambuliwa msikiti na kupigwa wanachama wa CCM tukio limetokea  alfajiri ya jana Jumanne tarehe 22 Septemba 2020, tumeanza opereshehni  na watu 22 tumewashikilia.”

Kamanda Khamis amesema, Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Tunahoji baadhi ya viongozi wa wilaya wa ACT, tunawahoji kwa nini wanachama wenu wanafanya fujo wanaingia msikitini kushambulia, tuaendelea na upelelezi kwa yeyote anahisi kuna jambo limetokea ni vyema kuripoti sisi jukumu letu ni kulinda usalama wa raia,” amesema Kamanda Khamis ambaye hakuwa tayari kuwataja majina yao

Kuhusu  hali za wanachama watatu wa CCM waliojeruhiwa msikitini, Kamanda Khamis amesema, mmoja ameruhusiwa kurudi nyumbani huku wawili wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Magharibi Unguja.

“Waliojeruhiwa vibaya ni wawili, taarifa mwanzo ni watatu lakini mmoja ameruhusiwa aliparazwa na panga, mmoja alikatwa sehemu ya koo mmoja amemumia mkono, wawili hao hospitali wamehamishiwa Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Magharibi,” amesema Kamanda Khamis.

Kamanda huyo wa Polisi Kaskazini Pemba amewaonya wanasiasa na wafuasi wao kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani katika kipindi cha kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Kamanda Khamis amesema atakayejaribu kujihusisha na vitendo hivyo atapambana na Jeshi la Polisi.

“Hiki kipindi cha kampeni tunakwenda katika uchaguzi,  wananchi kwa ujumla wanaojihusisha na uhalifu dhidi ya masuala ya siasa waache mara moja na yeyote atakayekiuka maagizo haya sheria zipo, yoyote atakayejaribu kuharibu amani tutapambana nae,” ameonya Kamanda Khamis.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!