Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe awataka wananchi kumuuliza Magufuli maswali 4
Habari za Siasa

Membe awataka wananchi kumuuliza Magufuli maswali 4

Benard Membe, Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo
Spread the love

BERNARD Membe, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, amewataka wananchi wa Kilwa Mkoa wa Lindi, kuumuuliza maswali manne, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais John Pombe Magufuli. Anaripoti Faki Sosi, Lindi … (endelea).

Mwanadiplomasia huyo, ameyatoa maswali hayo kwa wananchi wakati akihutubia mkutano wa kampeni za urais uliofanyika leo Jumatano tarehe 2 Septemba 2020 katika viwanja vya Bustani ya Mkapa, Kilwa Masoko.

Membe aliyepata kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kati ya mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema, Rais Magufuli atakapofika Kilwa aulizwe maswali hayo.

Baadhi ya maswali hayo, Membe amesema, iko wapi mipango ya gesi kwa wananchi wa Kilwa, Lindi na Mtwara na akijibu swali hilo aulizwe jingine.

“Kwanini mikoa ya Kusini hakuna barabara ya kudumu, kwani hakuna barabara ya kutoka njia panda kwenda Pande kwa sababu alikuwa waziri wa Ujenzi na Miundombinu,” amesema Membe

Pia, Membe amesema swali jingine “tumuulize kwanini ameingilia soko la korosho, ufuta na mbaazi.”

Amesema, mawakala wa korosho maarufu kama kagomba atawaruhusu kufanya biashara endapo watamchagua katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Kuhusu suala la uvuvi,Membe ameahidi kukuza maslahi ya uvuvi pamoja na kuzuia kuwachomea nyavu wavuvi.

Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

“Mimi sitachoma moto nyavu zenu, mtavua samaki, hayupo atakayechoma moto nyavu kama ni Waziri nitamfukuza siku hiyo hiyo. Huku akiwauliza wananchi nilonge nisilonge nao wakimjibu..longa” amesema Membe

Awali, mgombea mwenza, Profesa Omar Fakih Hamad amesema, ili taifa listawi ni lazima kuimarisha muungano kupitia chama hicho.

Amesema, ili safari ya maendeleo ya Taifa ni lazima kuwepo kwa muungano wa haki.

Profesa Hamad amesema, ili Muungano uwe na haki kwa pande zote kati ule wa Tanzania Visiwani na Tanzania Bara ni lazima wakiondoe Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.

Mkutano Mkuu wa CCM

Amesema ujumbe huo ametoka nao Visiwani Zanzibar na kwamba kuiondoa CCM kutastawisha Muungano wenye haki.

Amewataka wapiga kura waichague ACT-Wazalendo kwa kuwa chama hicho kina nguvu na kwamba CCM imechoka.

“Punda akiwa mbovu hata ukibadirisha masogi mara  kumi hataweza kuimarika . ACT-Wazalendo ni punda mzima,” amesema

Amesema Membe atakapoingia madarakani atahakikisha Muungano utakuwa wenye haki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!