Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu amwachia swali Magufuli 
Habari za SiasaTangulizi

Lissu amwachia swali Magufuli 

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amemtaka Rais John Magufuli aeleze ukweli kuhusu watu waliohusika kutaifisha migodi ya madini ya wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga … (endelea).

Lissu ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 2 Septemba 2020 katika mkutano wa kampeni za urais mkoani Shinyanga.

Lissu amemtaka Rais Magufuli ambaye ni mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, kesho Alhamisi tarehe 3 Septemba 2020 atakapofanya kampeni mkoani humo, awaeleze Watanzania waliohusika na ugawaji wa madini ya Watanzania.

Amesema, Chadema haijawahi kuwa madarakani na haiwezi kuhusika kwa lolote na kwa kipindi chopte, Serikali ya CCM ndiyo inahusika na kukabidhi madini ya wananchi wa Mwanza, Shinyanga na Wananchi kwa wazungu.

“…halafu leo anakuja anasema mkimpa Lissu atatoa madini yetu kwa mabeberu, kwani yapo? Ni ya kwenu au wameshayagawa yote,” amehoji Lissu na kuibua shangwe uwanjani hapo.

Lissu amewaomba kura wananchi wa Kanda ya Victoria akieleza kwamba, alikuwa mstari wa mbele kutetea masilahi yao hasa wachimbaji wadogo wa madini.

Chadema

“Wakati mnafukuzwa Nyamongo aliwasemea nani, mimi nilisema nikakamatwa, nikalala ndani nikashtakiwa kwa uchochezi, tuambieni ukweli, aje kesho aseme alikuwa wapi wakati kilio kikubwa kinawakuta watu wa Shinyanga,” amesema Lissu.

Wakati huo huo, Lissu amejinadi kama atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, Serikali yake itatibu majeraha ya wachimbaji wadogo wa madini pamoja na wakulima

“Serikali ya Chadema itakuwa serikali ya haki, tutatibu majereha haya ya wafugaji wa Shinyanga, tutatibu majeraha ya wakulima wa pamba wa Shinyanga, tutafuta machozi ya wafugaji wadogo wa nchi nzima,  tutatenda haki sababu haki huinua Taifa,” amesema Lissu.

Aidha, Lissu amesema katika Serikali yake, hataruhusu wakulima wakopwe mazao yao na wafanyabiashara.

“Serikali ya Chadema, itapiga marufuku mtu yoyote au kampuni yoyote ambayo itakopa pamba au korosho au zao lolote la wakulima wetu, tunataka wakulima wetu popote walipo watendewe haki,” amesema Lissu

Hali kahalika, Lissu ameahidi kulinda haki za wakulima na wafugaji kwa kuhakikisha wanatekeleza shughuli zao bila kubughuziwa.

“Serikali ya Chadema wafugaji wa Shinyanga au eneo lingine lolote akamatiwe mifugo yake ama afungwe,  tutahakikisha tunatengeneza utaratibu na hii inawezekana, utaratibu ambao utawezesha kuchunga kwenye hifadhi wakati wa shida ya maji au majani,” amesema Lissu.

Lissu kesho atakuwa mkoani Tabora na Rais Magufuli ambaye leo alikuwa Tabora kesho atakuwa Shinyanga.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

error: Content is protected !!