May 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo waja 50 kwa 50

Dorothy Semu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Bara

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania kimesema, endapo kitaingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 20200, kitaweka usawa wa kijinsia wa 50 kwa 50 kwenye uongozi. Anaripoti Faki Sosi, Lindi … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatano tarehe 2 Septemba 2020 na Dorothy Semu, Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo kwenye mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Bernard Membe kwenye viwanja vya Bustani ya Mkapa Kilwa Masoko.

Doroth amesema, chama hicho ndio chama pekee kitakachotekeleza sera ya 50 kwa 50 kwenye nafasi za uongozi kati ya wanaume na wanawake.

“Miaka mitano imekuwa michungu kwa wanawake wa Tanzania, ACT-Wazalendo itampa mwaname wa kitanzania heshima na kwamba  ACT-Wazalendo, tunasema 50 kwa 50 wanawake na kwamba wanawake wanaweza,” amesema Doroth.

error: Content is protected !!