Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yaiteka nchi, mashabiki waitika
Michezo

Yanga yaiteka nchi, mashabiki waitika

Spread the love

IDADI kubwa ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwenye kilele cha “Wiki ya Mwananchi” kinaweza kuwa kielelezo tosha cha kuonesha kufanikiwa kwa tamasha hilo ambalo lilijumuisha burudani za muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali, lililofanyika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam wenye uwezo wa kubeba watu 60,000. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Tamasha hilo ambalo limefanyika kwa mwaka wa pili na kuonesha mafanikio makubwa kiasi cha mashabiki kuutapisha Uwanja huku lengo kuu likiwa kuwakutanisha mashabiki wa timu hiyo pamoja na kutambulisha wachezaji watakao kwenda kutumika kwenye msimu uajo wa Ligi na mashindano mengine.

Tamasha hilo lilianza majira ya saa 4 asubuhi kwa kujumisha burudani mbalimbali kiasi cha kuvutia waliowengi kwa kufuatilia kupitia matangazo ya televisheni.

Mashabiki walijitokeza kwa wingi kuja kuona usajili mpya wa wachezaji uliofanywa na uongozi wa klabu hiyo katika siku za hivi karibuni na kufufua tena matumaini yao kwenye kulinyaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao.

Kitendo cha Yanga kuujaza uwanja huo, kimetoa jibu kwa watani zao walioshindwa kuujaza kwenye kilele cha “Simba Day.”

Huwenda likawa ni moja ya tukio lililofuatilia na idadi kubwa ya watu nje na ndani ya mipaka ya Tanzania kutokana na ukubwa wa mpira wa Tanzania ulipofikia kwa sasa.

Ukiacha uwanja kujaa  sehemu ya ndani, idadi kubwa ya mashabiki ilikuwa nje ya uwanja.

Ikumbukwe mpaka Yanga inahitimisha “Wiki ya Mwananchi” bado hawajatambulisha jezi watakazo tumia katika msimu ujao wa mashindano uliozinduliwa jana Jumapili jijini Arusha kwa mchezo wa Ngao ya Jamii uliozikutanisha Simba na Namungo na Simba kuibuka mshindi kwa 2-0.

Katika mchezo wa jana kati ya Yanga na Aigle Noir ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa 2-0 huku mchezaji aliovutia mashabiki wengi ni nyota kutoka Angola, Calinhos pamoja na Tuisila Kisinda na Tunombe Mukoko, wakitokea Congo

 

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

Michezo

Unakosaje pesa ukiwa na Meridianbet leo

Spread the love Alhamisi ndio hii sasa mteja wa meridianbet ambapo leo...

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

error: Content is protected !!