Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majimbo 20 wapinzani njia panda
Habari za SiasaTangulizi

Majimbo 20 wapinzani njia panda

Spread the love

TAKRIBANI majimbo 20 ya ubunge Tanzania Bara, yapo njia panda baada ya wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutajwa kupita bila kupingwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa za awali zinaeleza, majimbo hayo yaliopo kwenye mikoa mbalimbali nchini, wagombea wa upinzani hawakupitishwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokidhi masharti.

Hata hivyo, Dk. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa (NEC) akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano tarehe 26 Agosti 2020 jijini Dodoma amesema, licha ya kuwepo kwa taarifa hizo, lakini tume haijatangaza rasmi hatma ya uteuzi wa wagombea hao kwa kuwa, kuna nafasi ya pingamizi kutoka kwa wagombea.

“Jana Agosti 25 tume ilikamilisha zoezi la uteuzi wa wagombea kiti cha urais na makamu wa urais, ubunge na udiwani nchi nzima, mpaka sasa tume haijatupewa taarifa yoyote juu ya zoezi hili muhimu, tayari vyombo vya habari kadhaa vinaaza kutoa matokeo ya uteuzi huu,” amesema Dk. Mahera.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi NEC amesema, ni mapema mno kutangaza wagombea wamepita bila kupingwa, kwa kuwa lolote linaweza kujitokeza kwani wagombea wana nafasi ya kuwekeana pingamizi.

“Unapotangaza mtu amepita bila kupingwa, hiyo inaweza kupelekea uvunjifu wa amani pale mtu anapokuwekewa mapingamizi, isionekane ameshindaisha. Mimi mwenyewe mkurugenzi wa uchaguzi sijapata majina hayo rasmi.

“Kama mtataka matokeo, tutawapatieni taarifa hiyo kutoka tume, kabla ya kuweka mapingamizi vyombo vimeanza kuweka matukio na vinaweza kuchukuliwa hatua za kisheria, kuweni makini, mnaweza kuchochea vurugu na uhasama,” amesema Dk. Mahera.

Hata hivyo, tayari vyama vya siasa vya upinzani ikiwemo Chama cha Wananchi (CUF) na ACT-Wazalendo, vimezitaka mamlaka husika kutatua changamoto hiyo, huku vikiahidi kukata rufaa katika maeneo ambayo wagombea wa CCM wamepita bila kupingwa.

Emmanuel Simvula, Meneja Kampeni wa Taifa wa ACT-Wazalendo, ametangaza kuweka pingamizi katika maeneo ambayo CCM ‘amedaiwa kupita bila kupingwa.

Mhandisi Mohammed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari wa CUF ametoa wito kwa mamlaka husika kuingilia kati suala hilo.

Miongioni mwa wagombea ambao wanadaiwa kupita bila kupingwa ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, Vwawa-Songwe; Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, Ushetu – Simiyu; Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa, Ruangwa, Lindi.

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama

Hadi leo, Mkoa wa Morogoro na Dodoma ndio inayongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagombea wa CCM walitajwa kupita bila kupingwa, kila mkoa una wagombea sita.

MwanaHALISI ONLINE imetamfuta kwa simu Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa CCM mkoani Morogoro ambaye amethibitisha wagombea ubunge sita wa chama hicho kwenye mkoa wake, ‘wamepita’ bila kupingwa.

Amesema, CCM mkoani Morogoro kilipewa taarifa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo husika ya kwamba, wagombea wake wamepita bila kupingwa.

“Kwa mujibu wa wasimamizi wa uchaguzi, tumepokea kuwa wagombea wetu sita wamepita bila kupingwa, chama kimepokea taarifa rasmi na tumefuatilia jana na kwenye zoezi la uteuzi tulikuwepo pale, tuliona ni kweli watu wamebandikwa, tumejulishwa na tumethibitishiwa ni kweli wamepita bila kupingwa,” amesema Shaka.

Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Wagombea wanaotajwa kupita bila kupingwa Morogoro ni Hamis Taletale ‘Babu Tale,’ Morogoro Kusini Mashariki; Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Palamagamba Kabudi, Kilosa; Abdulaaziz Abood, Morogoro Mjini.

Ahmed Shabiby, Gairo, Morogoro; Jonas Vanzland, Mvomero, Morogoro na Innocent Kalogeris, Morogoro Kusini.

Dodoma; wanaodaiwa kupita bila kupingwa ni Spika Job Ndugai, Kongwa; Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya vijana, Anthony Mavunde, Dodoma Mjini; Deo Ndejembi, Chamwino. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji, Kondoa vijijini na George Malima, Mpwapwa.

Kwenye maeneo mengine Tanzania wamo Alexander Mnyeti (Misungwi); Vita Kawawa, Namtumbo; Shanif Mansoor, Sumve,Mwanza; Joseph Kamonga, Ludewa, Nape Nnauye, Mtama, Lindi na Geofrey Mizengo Pinda, Kavuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!