Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu kuwawekea pingamizi wagombea urais
Habari za SiasaTangulizi

Lissu kuwawekea pingamizi wagombea urais

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, akiwasilisha fomu za pingamizi kwa wagombea wengine wa nafasi ya urais
Spread the love

TUNDU Lissu, Mgombea urais wa Tanzania, amewasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wengine wa urais walioteuliuwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Jana Jumanne tarehe 25 Agosti 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliwateua wagombea 15 akiwemo Lissu kuwania urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.

Baada ya uteuzi huo, huwa kuna fursa ya watu wanaoruhusiwa kisheria ikiwemo wagombea, kuweka pingamizi kabla ya saa 10 jioni leo Jumatano tarehe 26 Agosti 2020.

Lissu akiwa na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu, wanachama na viongozi wengine wa Chadema amewasili ofisi za NEC jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumain Makene imesema Lissu na Mwalimu anawasilisha “fomu zake za mapingamizi dhidi ya wagombea wengine katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

“Baada ya hapo, atazungumza na waandishi wa habari Ofisi za Chadema, Kanda ya Kati, jijini Dodoma,” amesema Makene.

Pamoja na Lissu, wengine walioteuliwa ni; Rais John Pombe Magufuli (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa (SAU), Cecilia Augustino Mwanga (Demokrasia Makini), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi) na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF.

Pia wamo, Philip John Fumbo (DP), Bernard Membe (ACT- Wazalendo), Qeen Cuthbert Sendiga (ADC), Twalib Ibrahim Kadege (UPDP), Hashimu Rungwe (Chaumma), Khalfan Mohamed Mazurui (UMD) na Seif Maalim Seif (AAFP).

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wananchi Dar watakiwa kujitokeza barabarani kumuaga Hayati Mwinyi

Spread the loveWANANCHI wasiokuwa na muda wa kwenda katika Uwanja wa Uhuru,...

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

error: Content is protected !!