Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yamteua Membe kugombea urais Tanzania  
Habari za Siasa

NEC yamteua Membe kugombea urais Tanzania  

Bernard Membe, Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya ACT-Wazalendo akirudisha fomu ya kuwania kiti hicho
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Bernard Membe kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo na mgombea mwenza, Profesa Omar Fakih Hamad kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Membe na mgombea wake mwenza, Profesa Hamad wameteuliwa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage katika ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.

Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kati ya mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, amekuwa mgombea wa tisa kuteuliwa na tume hiyo.

Wagombea wengine waliokwisha rejesha fomu na kuteuliwa ni; Rais John Pombe Magufuli (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa (SAU), Cecilia Augustino Mwanga (Demokrasia Makini), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi), Ibrahim Lipumba (CUF)  na Philip John Fumbo wa DP.

Vyama vilivyojitokeza kuchukua fomu vilikuwa 17 na mpaka sasa vimerejesha tisa bado nane. Mwisho wa urejeshaji kwa mujibu wa NEC ni saa 10 jioni.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!