May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rungwe ateuliwa kugombea urais Tanzania

Hashim Rungwe wa chana cha Chaumma kugombea urais wa Tanzania akirudisha fomu za kuwania kiti hicho

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Hashim Rungwe wa chana cha Chaumma kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. Rungwe amekuwa mgombea wa 12 kuteuliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rungwe ameteuliwa leo Jumanne tarehe 28 Oktoba 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage katika ofisi za tume hiyo jijini Dodoma.

Rungwe amekuwa mgombea wa 12 kati ya 17 waliochukua fomu, kurejesha na kuteuliwa na tume hiyo.

Kati ya wagombea hao 12, wawili ni wanawake ambao ni; Qeen Cuthbert Sendiga wa chama cha ADC na Cecilia Mwanga wa chama cha Demokrasia Makini.

Wagombea wengine waliokwisha rejesha fomu na kuteuliwa ni; Rais John Pombe Magufuli (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa (SAU), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi), Ibrahim Lipumba (CUF), Philip John Fumbo (DP), Twalib Ibrahim Kadege (UPDP) na Bernard Membe wa ACT-Wazalendo.

Baadhi ya vyama ambavyo havijarejesha fomu ni vitano, Chadema, AAFP na CCK.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

error: Content is protected !!