Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Morrison atoa ya moyoni kuhusu Simba
Michezo

Morrison atoa ya moyoni kuhusu Simba

Spread the love

KIUNGO mshambuliaji wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison amesema kuwa klabu ya Simba ndio chuo cha mpira wa miguu nchini Tanzania na hakuna klabu nyingine. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezaji huyo ameyasema hayo wakati alipotambulishwa kwenye Tamasha la klabu hiyo maarufu kama ‘Simba Day’ lilofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam alipopewa nafasi ya kuongea na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara mbele ya umati wa mashabiki wa Simba waliojitokeza huku akisema kuwa anaipenda sana timu hiyo.

“Naipenda Simba, kwani ndio chuo kikuu cha mpira wa miguu Tanzania na hakuna klabu nyingine,” alisema Morrison.

Mchezaji huyo ambaye amesajiliwa na klabu ya Simba akitokea Yanga baada ya mvutano wa muda mrefu na viongozi wa timu juu ya uhalali wa mkataba wake na baadae kamati ya Haki na Hadhi za Wachezaji kutoa uwamuzi ya mchezaji huyo kuwa huru baada ya kusikiliza shauli hilo.

Mchezaji huyo ambaye alikuja nchini January 2020 kujiunga na klabu ya Yanga kwa mkataba wa miezi sita na baadae kutimkia Simba ambapo amesaini makubaliano ya mkataba wa miaka miwili.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!