Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ummy: Nitafanya kampeni kitanda kwa kitanda, uvungu kwa uvungu
Habari za Siasa

Ummy: Nitafanya kampeni kitanda kwa kitanda, uvungu kwa uvungu

Mgombea Ubunge Tanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ummy Mwalimu akikabidhiwa fomu
Spread the love

MGOMBEA Ubunge Tanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ummy Mwalimu amesema, atafanya kampeni shuka kwa shuka, kitandanda kwa kitanda na uvungu kwa uvungu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Ummy ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 22 Agosti 2020 mara baada ya kuchukua fomu ya kuteuliwa kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu 28 Oktoba 2020.

Ummy amewashukuru halmashauri kuu ya CCM kwa kumwamini na kumteua kuwania Jimbo la Tanga Mjini ambalo lilikuwa likiongozwa na Chama Cha Wananchi (CUF).

Huku akishangiliwa na mamia ya wana CCM waliomsindikiza kuchukua fomu,
ameahidi kufanya kampeni za kiistarabu shuka kwa shuka, kitanda kwa kitanda na uvungu kwa uvungu, “kuhakikisha jimbo linarudi katika chama cha mapinduzi CCM.”

Amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Tanga ambao walimpitisha kwa kura za kishindo kwa kumpendekeza kuwa mgombea ubunge.

“Wajumbe wamekuwa ni watu maarufu sana lakini wajumbe wa mkutanbo mkuu wa Tanga mjini kwangu mimi wamenitendea haki.”

“Kwangu mimi wamenipa heshima niwashukuru sana, wenyeviti wa CCM kutoka matawi yote 153 ya jiji la Tanga, makatibu tawi wote na makatibu wenezi wote pamoja na wajumbe waliotoka kwenye ngazi ya matawi,” amesema Ummy.

Amesema, “nimepata heshima ya kuwa mbunge viti maalumu miaka kumi na mshahara wa mbunge wa viti maalumu na jimbo ni mshahara mmoja. ningekuwa nimeshamaliza mchezo lakini kwasababu ya shauku na mapenzi makubwa kwa wanantanga hulka na hamu yangu ya kuipenda Tanga mjini ninataka kuiona yenye heshima na hadhi yake,” amesema.

Ummy ametuma salamu kwa wapinzani wake kuhakikisha wanajipanga vyema kwani wao watafanya kampeni za maendeleo na kampeni za kistaarabu na heshima kampeni zinazoakisi hadhi, utu na heshma ya wanatanga kutokana na hulka ya wanatanga kuwa wastaarabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!