Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe awakaribisha ACT-Wazalendo waliokatwa CCM
Habari za Siasa

Membe awakaribisha ACT-Wazalendo waliokatwa CCM

Benard Membe, Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo
Spread the love

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia chama cha upinzani ACT-Wazalendo, Bernard Kamillius Membe, amewakaribisha ndani ya chama hicho wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa kuwania ubunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kati ya mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawala wa awamu ya nne wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa ukaribisho huo jana Alhamisi tarehe 20 Agosti 2020.

Mwanadiplomasia huyo mashuhuri nchini aliyejiunga na ACT-Wazalendo tarehe 7 Julai 2020 baada ya kufukuzwa ndani ya chama alichokulia cha CCM amesema, waliokatwa ndani ya chama hicho kuwania kugombea ubunge wajiunge na ACT-Wazalendo.

Jana Alhamisi, CCM ilitangaza majina ya walioteuliwa kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 huku ikishuhudia zaidi ya wabunge 70 wakishindwa kutetea nafasi zao.

https://twitter.com/BenMembe/status/1296562904431558658

Membe akitumia ukurasa wake wa Twitter ameandika “uteuzi wa CCM uliofanywa leo (jana) umenifurahisha sana! Nawapongeza wote waliobahatika kuteuliwa, lakini kubwa zaidi nawapa pole wale wote waliokatwa kwa sababu ya kuwa karibu nami.”

           Soma zaidi:-

“Hiyo ni baraka siyo balaa. Karibuni mjiunge na ACT- Wazalendo haraka ili safari iendelee!” ameandika Membe ambaye ni Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!