Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Panga la CCM lafyeka vigogo 75
Habari za SiasaTangulizi

Panga la CCM lafyeka vigogo 75

Rais John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM
Spread the love

WABUNGE takribani 75 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao walijitosa kutetea nafasi zao katika uchaguzi mkuu wa 28 Oktoba mwaka huu, wameangukia pua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Miongonu mwa wabunge walioangukia pua kwa kushindwa kupitishwa na chama hicho, baadhi Yao waliongoza kwenye kura za maoni, wengine walishika nafasi za pili na wapo walioshika nafasi ya tatu.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC), uliopitisha majina ya wagombea hao, umefanyika leo Alhamisi, tarehe 20 Agosti 2020 chini ya mwenyekiti wake, Dk. John Magufuli.

             Soma zaidi:-

Kati ya wabunge hao, yumo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe; Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa.

Taarifa zinasema, katika orodha ya wabunge 264 -kwa maana ya majimbo 214 (Bara) na 50 ya Zanzibar – wamo wabunge wakongwe na maarufu, “waliokatwa.”

Mathalani, aliyepata kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, waziri wa miundombinu na mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, pamoja na kwamba alishinda kura za maoni katika jimbo lake la Bariadi Mashariki, lakini hakuteuliwa.

Wengine, ni mbunge wa miaka mingi na waziri wa zamani wa nishati na madini, William Ngeleja (Sengerema); aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba na aliyekuwa mbunge wa Busega, Raphael Chegeni.

Katika orodha hiyo, kuna wabunge wa viti maalum walioshindwa kura za maoni kwenye majimbo, akiwamo Angella Kairuki (Same Mashariki); Vick Kamata, aliyekuwa anataka kuligomboa jimbo la Kibamba na Halima Bulembo.

“Hizo ni sura ambazo hazitoonekana ndani ya Bunge la 12 labda waingie kwa uteuzi wa nafasi kumi za Rais. Na hata kama wataingia, basi hawatakuwa wote, kwa kuwa sheria inampa rais nafasi 10 tu, kuteuwa wabunge,” ameeleza mchambuzi mmoja wa kisiasa ambaye hakupenda kutajwa jina.

Wengine walioshindwa kupenya, ni Charles Tizeba (Buchosa), Balozi Adad Rajab (Muheza), Balozi Diodorus Kamala (Nkenge),Stephen Masele (Shinyanga Mjini), Julius Kalanga (Monduli), Maulid Mtulia (Kinondoni), Lolesia Bukwimba (Busanda), Juma Nkamia  (Chemba), Chacha Ryoba (Serengeti) na Albert Obama (Buhigwe).

Wengine, ni Daniel Nsanzugwanko (Kasulu Mjini), Mbaraka Bawazir (Kilosa), Goodluck Mlinga (Ulanga), Suleiman Ahmed Saddiq (Mvomero), Abadallah Mtolea (Temeke), Haroon Pirmohamed (Mbarali), Rafael Gashaza (Ngara), Prof. Jumanne Maghembe (Mwanga), Hassan Masala (Nachingwea), Jitu Soni (Babati Vijijini) na Isaay Paulo (Mbulu Mjini).

Wamo pia, James Ole Millya (Simanjiro), Emmanuel Papian (Kiteto), Omar Badwel (Bahi), Issa Mangungu (Mbagala), Augustino Masele (Mbogwe),  Venance Mwamoto (Kilolo), Godfrey Mgimwa (Kalenga), Mahmoud Mgimwa (Mufundi Kaskazini), Edwin Sannda (Kondoa Mjini) na Charles Kitwanga (Misungwi).

Dk. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo

Wengine, ni Oscar Mukasa (Biharamulo Magharibi), Dk. Pundenciana Kikwembe (Kavuu),   Richard Mbogo (Nsimbo), Christopher Chiza (Buyungu), Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini), Prof. Noman Sigalla (Makete), Kangi Lugola (Mwibara), Deogratias Ngalawa (Ludewa), Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na William Dau (Nanyumbu).

Wengine, ni Dk. Mary Nangu (Hanang),  Hasna Mwilima (Kigoma Kusini), George Lubeleje (Mpwapwa), Joel Mwaka (Chinolwa) sasa Chamwino;  Jerome Bwanausu (Lulindi), Rashid Chuachua (Masasi), Saul Amon (Rungwe), Peter Lijualikali (Kilombero), Nimrod Mkono (Butiama) na Victor Mwambalaswa (Lupa).

Katika orodha hiyo, wapo pia Dk. Shukuru Kawambwa (Bagamoyo), Dk. Haji Mponda (Malinyi), Omary Kigoda (Handeni Mjini), Mary Chatanda (Korogwe Mjini), Mboni Mhita (Handeni Vijijini), Edward Mwalongo (Njombe Mjini), Joram Hongoli (Lupembe), Greyson Lwenge (Wanging’ombe), Dk. Dalaly Kafumu (Igunga), Mussa Ntimizi (Igalula) na   Ezekiel Maige (Msalala).

Peter Lijualikali (kulia) akipokea fomu ya kuwania ubunge jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM

Wengine, ni Allan Kiula (Iramba Mashariki), Justin Monko (Singida Kaskazini), Janet Mbene (Ileje),  John Kadutu (Ulyankulu) na Prof. Anna Tibaijuka (Muleba Kusini) , Salum Khamis (Meatu) na Daniel Mtuka (Manyoni Mashariki), Salum Khamis (Meatu) na Daniel Mtuka (Manyoni Mashariki).

Kupatikana kwa taarifa kuwa robo ya wabunge wa CCM wameenguliwa na chama chao; na au wamelazimishwa na wajumbe kustaafu, kunatokana na hatua ya NEC ya chama hicho, kuwapigia mstari mwekundu.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa NEC, Dk. Magufuli alisema, kabla ya majina ya wagombea hao kupelekwa kwenye kikao hicho, yalifanyiwa uchambuzi wa kina na vikao vya Sektarieti, Kamati Kuu (CC) na Kamati ya Maadili na usalama.

Dk. Magufuli alisema, vikao hivyo vilitumia taarifa nyingi kutoka vyanzo mbalimbali na yeye mwenyewe akasema, alisoma majina yote 10,367, na kwamba amekusanya uchambuzi wa kina kwa kila mgombea.

Anna Tibaijuka, Mbunge wa Muleba Kusini

Alisema, “ndio maana uchambuzi wa kila mgombea, mmoja baada ya mwingine, tunao hapa. Atakayetaka ufafanunuzi wa mtu yoyote tutampa, lakini kamati kuu, tulikaa na kuchambua ili kurahisha kazi ambayo mtaifanya leo.”

Aidha, hatua ya kutolewa kwa majina hayo, kumemaliza joto la wanachama wa CCM, waliojitosa katika kinyang’anyiro hicho cha kuwania ubunge wa majimbo na wa viti maalum.

Kikao cha CC kilifanyika Ikulu ya Chamwino, kwa siku mbili mfululizo, chini ya uenyekiti wa Rais Magufuli, kilipitia mafaili hayo ya wagombea kutoka Bara na Visiwani.

Katika kinyang’anyiro hiki, wanachama takribani 11,000 wa CCM, walijitosa kuwania nafasi za ubunge wa majimbo na viti maalum.

Katika uchaguzi wa mwaka huu, watakaokatwa CCM wana nafasi ndogo sana ya kupenya, kwa kuwa zitakuwa zimebaki siku nne kufungwa kwa pazia la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Tume ya uchaguzi imetangaza, tarehe 25 Agosti 2020, kuwa ndio siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu Vyama vingi vya siasa kama CUF, Chadema, ACT-Wazalendo na NCCR-Mageuzi, kwa sehemu kubwa wamekwisha kufanya uteuzi wa wagombea wao wa ubunge na hivyo kuwapa wakati mgumu wale watakaokatwa kuendeleza ndoto zao za kuwania nafasi hizo katika uchaguzi wa mwaka huu.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Alichokisema Rais Samia baada ya kupokea ripoti ya CAG, TAKUKURU

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itafanyia kazi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

Habari za SiasaTangulizi

Deni la Serikali laongezeka kwa trilioni 11

Spread the loveDENI la Serikali imeongezeka kwa takribani Sh. 11 trilioni sawa...

error: Content is protected !!